Picha: ujumbe wa Lowassa ukiwa katika ndege katika safari ya Bukoba kutembelea wahanga wa tetemeko la ardhi.
Kwanza nianze kwa kumpongeza Ndugu Lowassa kwa wasaa na mali yeye na ujumbe wake (TeamLowass) waliotoa kuchangia mifuko 400 ya saruji ambayo ni sawa na shilingi milioni 6 za kitanzania ikiwa mfuko mmoja utauzwa shilingi 15,000/-, ni pesa nyingi tu hakuna ubishi.
Ila kama wangepanga mipango vyema asingeongozana na kundi kubwa lililogharimu mamilioni, kiwango zaidi ya msaada waliotoa. Angeambatana na watu wachache ili angalau kubana matumizi na pesa nyingi ingeelekezwa kwa wahanga...., kwa mtu mkarimu haihitaji akili nyingi sana..ndio maana Rais Museveni wa Uganda aliona kuliko asafiri ni bora achangie dola 200,000/- ambapo angekuja Bukoba angetumia pesa nyingi zaidi.
Naum,ilikuwa ni muhimu Lowassa kwenda lakini angeambatana na ujumbe mdogo...haikuwa na haja ya kuambatana na ujumbe mkubwa uliolazimu kukodi magari na huduma mbalimbali na kibaya zaidi walitaka kila mtu katika mji wa Bukoba ajue uwepo wao.Kundi la wanahabari liliongozwa na Asiraji Mvungi kutoka ITV,Arusha,masheikh,manabii,wapambe na baadhi wanachadema akiwemo ndugu Lema mbunge wa Arusha Mjini. ambao waliripoti propaganda badala ya tukio, shukrani ziwaendee Azam Tv ambao ndio pekee walioripoti tukio la kifo cha kada wa CHADEMA aliyekufa akiwa na msafara kwa mazingira ya kutatanisha.
Hii inaweka alama kuwa hakika taifa lingetumbukia katika kadhia kubwa ya matumizi ya hovyo na ubadhirifu mkubwa wa mali za umma endapo Team Lowassa wangeingia madarakani na hapa Pongezi nyingi kwa Raisi Mstaafu na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mh.Jakaya Kikwete aliliona na kutuepusha na dhahama hii.
Mwisho msaada ule alioutoa ni kwa niaba ya CHADEMA au TeamLowassa...kwa sababu Mbowe ambaye ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA alienda Bukoba na kuondoka bila lolote zaidi ya kugomba na kubadili 'profile' kwenye akaunti zake za mitandao ya jamii.
Kiongozi mwenye busara,maono na mwenye kupenda wananchi wake hujinyima kwa ajili ya wananchi wake.....sasa kama leo CHADEMA/TeamLowassa wanatumia mamilioni kufanya safari na tambo za kifahari je wangekuwa na dhamana ya rasilimali za taifa ingekuwaje.