Msimu wa 2016/17 umeanza rasmi tangu wiki tatu zilizopita. Timu nyingi zimekuwa na mabadiliko makubwa katika mabenchi ya ufundi kwa kuajiri makocha wapya ambao wanaamini watawafikisha kwenye kilele cha mafanikio.
JOSE MOURINHO
Mreno huyo ameshaiongoza Manchester United kwenye michezo minne ya ushindani ikiwamo na Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City. Bado mbinu zake hazijafanikiwa sawasawa licha ya United kushinda michezo yote hiyo.
Kadri muda unavyosonga ndivyo United wanabadilika na kuwa timu ambayo Mourinho anaitaka.
PEP GUARDIOLA
Ameingia Manchester City msimu huu. Licha ya ugeni wake England amefanikiwa kuiongoza City kushinda michezo mitatu.
Falsafa yake ya kucheza mpira mzuri bado haijafanikiwa sana naye anahitaji muda ili timu yake ifuate kile anachohitaji.
ANTONIO CONTE
Ameachana na Timu ya Taifa ya Italia na kuelekea Stamford Bridge. Conte amefufua matumaini kwenye kikosi hicho ambacho msimu uliokwisha walishindwa kabisa kuonyesha cheche zao na mwishowe walimaliza nafasi ya 9.
Bado ana muda wa kuijenga Chelsea na kuifanya kuwa timu tishio Ligi Kuu England. Naye ameshinda michezo mitatu ya awali.
UNAI EMERY
Mmoja wa makocha waliofanikiwa kuiongoza Sevilla kwa mafanikio kwa kushinda kombe la kihistoria la Europa League. Emily sasa yupo PSG ambako bado hajafanikiwa kwa asilimia zote kuipa ushindi timu hiyo.
Emily ni muumini wa mpira wenye kasi ambao sasa ameupeleka pale jijini Paris. Anahitaji muda ili falsafa yake izoeleke. Hadi sasa ameshinda michezo miwili na kufungwa mmoja.
Mmoja wa makocha waliofanikiwa kufundisha timu nyingi barani Ulaya. Sasa Ancelloti anakinoa kikosi cha Bayern Munich ambacho kimeanza vyema kampeni zake za kutetea ubingwa wa Bundesliga.
Ancelloti ni muumini wa mpira mzuri na wenye kasi ambao umeonekana kushikwa mapema na wachezaji wake. Bayern Munich wana nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao.