test

Jumanne, 27 Septemba 2016

Hillary Clinton ni Kiboko, ampa mpasho huu Trump leo kwenye mdahalo.Soma mambo makuu yaliyoibuka kwenye mdahalo huo


HILLARY CLINTON ANA MIPASHO HATARI!



'A man who could be provoked with a tweet shouldn't have his fingers anywhere near the nuclear button' 


Ati mwanaume anayeropoka ovyo kwenye twitter vidole vyake havitakiwi sehemu yoyote iliyokaribu na swichi ya kubonyezea makombora ya Nuclear'
Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo.
Kura za maoni zinaonyesha wawili hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono.
Mambo mengine makuu yaliyoibuka kwenye madahalo:
  • "Umekuwa ukikabiliana na ISIS maisha yako yote,'' Bw Trump amemkejeli Bi Clinton
  • Amesema Bi Clinton hana uwezo wa kikudhibiti ukali wa kumuwezesha kuwa rais.
  • Wamarekani Weusi wanaishi "katika jehanamu" nchini Marekani, Trump amesema, kwa sababu maisha yao yamekuwa hatari sana.
  • Akijibu kupigwa risasi kwa watu weusi, bw Trump amesema suluhu ni kurejesha utawala wa sheria.
  • Bi Clinton amesema akichaguliwa kuwa rais atatekeleza mageuzi katika mfumo wa sheria kwa sababu "suala la asili limekuwa likiamua mengi".
  • Huu hapa ni muhtasari wa ukweli kuhusu baadhi ya masuala yaliyoibuka wakati wa mdahalo wa kwanza kwenye televisheni baina ya Hillary Clinton na Donald Trump.
  • Trump aliunga mkono uvamizi Iraq?
  • Madai: Clinton amedai Trump aliunga mkono uvamizi wa Iraq. Donald Trump ameendelea kusisitiza kwamba alipinga uvamizi uliofanywa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi Iraq mwaka 2003, na kusema madai ya Clinton kwamba aliunga mkono vita hivyo ni "upuuzi uliosambazwa naye (Clinton) kupitia vyombo vya habari".
    Msema kweli: Trump hakupinga hadharani vita hivyo kabla ya kuanza kwake. Septemba, 11 2002, mtangazaji wa redioni Howard Stern alimuuliza Trump iwapo alikuwa anaunga mkono wazo la kuvamia Iraq. Alijibu: "Naam, nafikiri hivyo". Kwenye mdahalo, amejaribu kufafanua akisema hakutoa jibu hilo kwa "uzito". Amesema faraghani, alimwelezea Sean Hannity wa Fox News, kwamba vita hivyo vingeathiri amani uthabiti Mashariki ya Kati, lakini hakuna ushahidi kwamba alifanya hivyo. Hata hivyo, alianza kuelezea shaka kuhusu uvamizi huo ulipoanza.

    Trump alipewa pesa na babake?

    MadaiClinton amemshambulia Trump kuhusu majitapo yake ya kuwa mweledi katika biashara. "Mnajua, Donald alikuwa na bahati sana maishani na yote hayo yalimfaa," Bi Clinton amesema. "Alianza biashara yake na $14m, alizokopa kutoka kwa babake."
    Msema kweli: Trump anasema alipokea mkopo wa $1m kutoa kwa babake. Pia alitumia pesa kutoka kwa urithi aliotarajia baadaye pamoja kama rehani katika kuchukua mikopo. Kadhalika, alirithi sehemu ya hisa kwenye biashara za babake.

    Mkataba wa Pasifiki

    MadaiTrump amedai kwamba Clinton aliwahi kusema Mkataba wa Kibiashara wa Pasifiki ni mkataba mzuri sana (wa "kiwango cha dhahabu") unaofaa kuigwa. Clinton amekanusha hilo lakini akaongeza: "Nilisema kwamba nilitumai ungekuwa mkataba mzuri."
    Msema kweliHapa Trump amepata. Clinton alienda hatua zaidi, na mwaka 2012 ziarani Australia alisema ulikuwa mkataba mzuri sana wa "kiwango cha dhahabu". "Mkataba huu wa TPP unaweza kiwango cha dhahabu katika mikataba ya kibiashara ya kufanikisha uwazi, uhuru na mazingira ya kibiashara ambayo yanaheshimu sheria na kusawazisha wadau wote."
  • Je, Clinton atachangia nafasi 10m za ajira?

    MadaiClinton amesema: "Watu wametazama mipango yetu wawili, na kuamua kwamba wangu utabuni nafasi za kazi 10 milioni na wako utatugharimu nafasi za kazi 3.5 milioni."
    Msema kweli: Clinton amewahi kudai hili awali. Madai yake yanatokana na kuangalia tathmini ya Moody Analytics ambayo ilisema nafasi 10 milioni za ajira zingebuniwa kwa kupanua uchumi. Iwapo mapendekezo yote ya Clinton ya kiuchumi yangetekelezwa, jambo ambalo ripoti hiyo inasema haliwezekani kwa urahisi, basi yanaweza kusaidia kuundwa kwa nafasi 3.2 milioni za kazi kati ya 10 milioni.
    Kampuni hiyo ilichanganua mipango ya Trump na kusema ingesababisha mdororo wa uchumi Marekani na kupotea kwa nafasi 3.5 milioni za ajira, jambo ambalo maafisa wa kampeni wa Trump wamepinga vikali.
    Lakini ripoti hizo zinaangazia vipindi tofauti. Mwandishi wa ripoti hizo Mark Zandi aliambia CNN Money kwamba ukilinganisha kwa njia nzuri, kukiundwa nafasi za kazi 10 milioni chini ya Clinton, sera za Trump zinaweza kuchangia kupotea kwa nafasi 400,000 pekee za ajira na si 3.4 milioni.

    Clinton amepambana na Islamic State maisha yake yote?

    Madai: Trump amejaribu mara kwa mara kumlaumu Hillary Clinton kutokana na kuwepo kwa wapiganaji wanaojiita Islamic State. Alijaribu tena wakati wa mdahalo, na kusema Clinton amekuwa akipambana na ISIS maisha yake yote ya utu uzima.
    Msema kweli:Haya ndiyo madai labda ya kushangaza zaidi mdahaloni. Clinton ana umri wa miaka 68. Kundi la Islamic State lilianza kusikika 2009, ingawa mizizi yake imo kwenye kundi la Kisunni la al-Qaeda nchini Iraq (AQI), lililoanzishwa 2004.

    Mabadiliko ya tabia nchi ni uongo wa Wachina?

    MadaiClinton amemtuhumu Trump kwa kusema kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni uongo uliobuniwa na Wachina. Amesisitiza "Sikusema hilo".
    Msema kweliMadai haya yanatokana na ujumbe wa Twitter alioandika 2012 ambao baadaye alisema alikuwa anafanya mzaha. Alisema: "Suala la ongezeko la joto duniani liliungwa na Wachina kwa ajili yao wenyewe ili kuzuia viwanda vya Marekani visiwe na ushindani."

    Ubaguzi wa rangi huongoza haki Marekani?

    MadaiClinton amesema suala la asili linaamua jinsi mtu anashughulikiwa katika mfumo wa mahakama Marekani.
    Msema kweli: Ni vigumu kubaini ukweli wa hili kwani hakuna takwimu rasmi. Lakini ukweli ni kwamba watu weusi hukamatwa na kuzuiliwa mara tano zaidi ukilinganisha na Wazungu. Wamarekani weusi ni asilimia 13 ya watu wote wa Marekani. Wazungu ni 64%. Lakini gerezani, weusi ni 40% na Wazungu 39%.
    Clinton pia amedai Wamarekani weusi wana uwezekano zaidi wa kuuawa kwa kupigwa risasi kuliko watu wa asili nyingine, suala ambalo linaungwa mkono na takwimu.

    Visa vya mauaji New York vimepanda au kushuka?

    Madai: Trump amedai kwamba visa vya mauaji New York yameongezeka.
    Msema kweli: Inategemea unaangalia vipi. Visa vya mauaji New York vimeshuka sana, lakini vilipanda kiasi kati ya 2014 na 2015, kwa mujibu wa takwimu za FBI. Lakini takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa idara ya polisi ya New York zinaonesha visa vya mauaji vilishuka 4% mwaka 2015.
    Lakini kwa jumla, visa vya mauaji vilipanda 10.8% mwaka 2015 Marekani, kiwango cha juu zaidi tangu 1971. Ongezeko kubwa lilitokea katika miji kadha ikiwemo Chicago, Washington DC na Baltimore.
    Trump pia amedai mbinu za "kusimamisha watu na kuwapekua" zimefanikiwa sana New York na kupunguza uhalifu.
  • Taarifa za ulipaji kodi za Trump

    MadaiTrump anasema hajatoa taarifa zake za ulipaji kodi kwa sababu kunafanyika utathmini wa kodi katika kampuni zake. Amesema kuzifichua kwa sasa huenda kusitoe maelezo ya kutosha.
    Clinton anasema Trump huenda asitoe taarifa hizo kamwe kwani zinaweza kufichua kwamba yeye si tajiri sana kama anavyojidai, halipi ushuru na hatoi pesa nyingi za kusaidia wasiojiweza kama anavyosema.
    Msema kweliKufanyiwa utathmini wa ulipaji kodi na Taasisi ya Mapato ya Marekani hakumzuii mtu kutoa taarifa zake za ulipaji kodi. Isitoshe, Trump hajawahi kutoa hadharani ushahidi wa kubaini kwamba anafanyiwa utathmini huo.
    Kwa mujibu wa jarida la Forbes, utajiri wa Trump ni $4.5bn, lakini yeye hudai utajiri wake ni $10bn.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx