Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.
Watu
walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana Jumapili wamesema mtu huyo
akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha kwenye gari kabla ya kuwekwa
kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki moja
iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini
jijini Dar.
“Aliyekufa
aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi walipiga
risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi walipomfyatulia
risasi na alikufa papo hapo,” amesema shuhuda wa tukio hilo na kuongeza kuwa
wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
atazungumzia tukio hilo leo
0 comments:
Chapisha Maoni