Tumeona uongozi wa WCB chini ya Diamond ukijitoa lawama kwa kuonyesha kuwa kuna makubaliano ya kuurudia huo wimbo baina yao na Dada Saida kupitia menejiment yake.
Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..
Diamond, mshike mkono Saida. Wajanja wasije wakatumia tena ujanja wa makaratasi wakamlaza njaa.