Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amezindua
treni ya pili ya abiria jijini Dar es Salaam, inayofanya safari zake
kuanzia kituo kikuu cha stesheni hadi Pugu.
Akizungumza
mara baada ya kuzindua treni hiyo Waziri Mbarawa amesema kuwa serikali
imejipanga usafiri huo kuwa endelevu ili kupunguza msongamano wa magari
katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri
Mbarawa amesema treni hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1500 kwa wakati
mmoja itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa msongamano na kuwahisha
shughuli za maendeleo kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Aidha
waziri Mbarawa amesema kuwa takribani magari 46 yanayobeba abiria 35
yatakuwa yamepungua kutokana na treni hiyo ambayo licha ya changamoto
zilizokuwepo ameahidi kushughulikia ili usafari huo uweze kudumu kwa
muda mrefu.