Mbunge
wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda
mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi,
Singida.
Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake.
Kukamatwa kwa Lissu
Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.
" Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.
“Kwa
hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa
kunipeleka. It’s likely (inawezekana) nitasafirishwa Dar usiku huu. In
fact (hakika) ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote
itakavyokuwa, there’s no turning back. There’s no shutting up (hakuna
kurudi nyuma, hakuna kunyamaza).
"Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail (niwe huru au jela)... Aluta continua!. "
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alithibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini alikataa kutoa sababu za hatua hiyo.
Chadema jana jioni ilitoa taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu ikisema: “Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.”

Taarifa
hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilibainisha
kuwa Polisi walimkamata jana jioni baada ya kumaliza mkutano wake wa
hadhara alioufanya Ikungi jimboni kwake na kueleza kuwa viongozi wa
chama hicho mkoani humo walikuwa polisi kuhakikisha anapata haki zake
kama inavyostahili na kwamba ofisi ya katibu mkuu inafuatilia kwa
ukaribu kujua sababu hasa ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka
kadri itakavyohitajika.
Lissu
amekuwa kwenye misukosuko na Jeshi la Polisi mara kadhaa na kwa siku za
karibuni alikamatwa na kufikishwa mahakamani akituhumiwa kutoa maneno
ya uchochezi kwenye gazeti la Mawio.
Sambamba
na kesi hiyo, Lissu alikamatwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno ya
uchochezi baada ya kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Msimamo wa Msigwa
Mkoani Iringa, Msigwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kwanza wa kibunge tangu alipochaguliwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, alisema hakuna wa kumpangia hoja za kuzungumza kwenye mikutano yake.

Juzi,
mbunge huyo alipewa barua na Jeshi la Polisi iliyoeleza kuwa imempa
kibali cha kufanya mikutano hiyo, lakini ikimuwekea masharti mbalimbali
likiwamo la kutozungumzia viongozi wengine na badala yake ajikite kwenye
shughuli za maendeleo na kuchukua maoni ya wananchi anaowawakilisha.
Pia,
alitakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu kutoka nje ya Mkoa wa Iringa au
eneo lolote lililo nje ya mamlaka atakayeruhusiwa kuzungumza.
Lakini jana akihutubia alisema: “Ninaona watu wote mna nyuso za hofu na mimi nimekuja kuwaondoa hofu …hakuna mtu mwenye mamlaka ya kunipangia cha kuzungumza, sipo hapa kwa matakwa ya polisi … mimi nipo kwa matakwa ya kisheria na ninazungumza kwa mamlaka mliyonipatia.

“Pia
Katiba inaeleza wazi mad raka na kinga ya Mbunge… mbunge anayo haki ya
kuitisha na kufanya mkutano wa hadhara kwa mjibu wa sheria.”
Kuhusu
Rais kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, Msigwa alisema hakubaliani na
hatua hiyo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni ukiukaji wa Katiba ya nchi na
Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambavyo nchi inayoongozwa chini
ya utawala wa kidemokrasia inapaswa kuvifuata.
“Ninamuunga
mkono na ninampongeza Rais John Magufuli kwa kupambana na ufisadi,
anapinga rushwa… lakini siungani naye kwa kitendo chake cha kukandamiza
demokrasia nchini na niwaombe wananchi wa Iringa kuungana na mimi
kumpinga mtu anayekandamiza demokrasia nchini,” alisema.
Kuhusu
Serikali kuhamia Dodoma, mbunge huyo ambaye pia ni waziri kivuli wa
Wizara ya Mambo ya Nje, alikosoa uamuzi huo akisema hajawahi kuona
katika mipango yote iliyowasilishwa na Serikali bungeni inayoelekeza
hilo.
“Serikali
ilileta mpango wake wa miaka mitano, mwaka mmoja na Bajeti, hivi vyote
vinaletwa bungeni na baada ya kujadiliwa na kupitishwa, vinatungiwa
sheria ili viweze kutekelezwa hivyo vipaumbele vyake ni lazima vifiti
kwenye mipango hiyo,” alisema Msigwa na kuongeza:
“Lakini katika vyote vitatu vya mwaka huu, mpango wa miaka mitano, mwaka mmoja na hata katika bajeti ya mwaka huu sijaona mahali popote palipoandikwa kipaumbele cha Serikali ni kuhamia Dodoma.”
“Lakini katika vyote vitatu vya mwaka huu, mpango wa miaka mitano, mwaka mmoja na hata katika bajeti ya mwaka huu sijaona mahali popote palipoandikwa kipaumbele cha Serikali ni kuhamia Dodoma.”
Msigwa
alisema kuhamisha Serikali ni gharama kubwa na kuwataka wakazi wa
Iringa na maeneo mengine kuhoji suala hilo kama ndicho kipaumbele cha
maendeleo na mahitaji yao.
Alisema wamejipanga kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo miradi ya barabara, kuboresha huduma za afya, usafi wa mazingira na miundombinu.
Alisema wamejipanga kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo miradi ya barabara, kuboresha huduma za afya, usafi wa mazingira na miundombinu.