Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku mikutano ya Operesheni
Ukuta iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia Septemba Mosi.
Akizungumza
katika kikao cha kazi kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama
mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, Makalla
alitangaza kupiga marufuku mkutano wowote utakaofanyika chini ya
utaratibu unaoitwa Operesheni Ukuta.
“Bila shaka wananchi wa Mbeya
wanataka amani na kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote wa
kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu wengine kutoka nje ya
mkoa,” alisema Makalla aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa CCM.
Alifafanua
kuwa wabunge na madiwani akiwamo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
(Sugu) wa Chadema wanaweza kufanya mikutano yao bila wasiwasi katika
maeneo yao.
Makalla
alisema vyombo vimewekwa tayari kuwashughulikia kwa nguvu zote
watakaokaidi maagizo yanayotolewa na kutoa mwito kwa vijana wa mkoa huo
kuwafichua watu wenye njama zozote zikiwamo za kuwahamasisha kufanya
maandamano au mikutano.
Polisi yadai kukamata vijana
Wakati Makalla akipiga marufuku Operesheni Ukuta, Polisi mkoani Mbeya wameeleza kuwakamata vijana wawili wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza ujumbe wa sauti wenye kauli za kutaka ofisi za CCM zichomwe moto.
Wakati Makalla akipiga marufuku Operesheni Ukuta, Polisi mkoani Mbeya wameeleza kuwakamata vijana wawili wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza ujumbe wa sauti wenye kauli za kutaka ofisi za CCM zichomwe moto.
Kamanda
wa Polisi mkoani hapa, Dhahir Kidavashari alidai kwamba vijana hao
waliandaa na kusambaza ujumbe huo Julai 29 ukiwataka vijana wenzao ambao
ni wanachama wa chama hicho kwenda kuchoma moto ofisi za CCM mahali
walipo.
Kidavashari
alidai kwamba ujumbe huo unahamasisha vijana kufanya uhalifu huo wakati
wowote kabla ya Septemba Mosi na baada ya hapo ilimradi nchi iwe kwenye
machafuko.
“Baada
ya kufuatiliwa na kumkamata, mtuhumiwa wa kwanza alipekuliwa na kukutwa
na simu ambazo zilitumika kusambaza ujumbe huo.Pia kupitia mtuhumiwa
huyo tulifanikiwa kumpata mtuhumiwa mwingine.”