Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo.
Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.
Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo. Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.