Waziri
wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewaambia askari wa jeshi la
Polisi mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na sheria bila kumuonea
mtu yeyote hasa wanyonge.
Waziri
Mwigulu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea makazi ya
watanzania wapya pamoja na kuzungumza na askari wa jeshi la polisi,
Magereza pamoja na Uhamiaji.
Mhe.
Mwigulu amesema kuwa Askari hao waondokane na tabia ya matukio ya
kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na kuwaonea na kusema kuwa
serikali kali ya awamu ya tano haitamfumbia macho askari atakayebainika
kufanya hivyo.
Aidha
Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema
kuwa serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti itakavyoruhusu ili
waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi.