Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, amepiga STOP maandamano ya UVCCM yaliyokuwa yafanyike nchi nzima Tarehe 31 August katika hali ya kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dk John Magufuli katika utendaji wake wa Kazi na kumshukuru Rais aliyemaliza muda wake Dk Jakaya Kikwete kwa kuiacha nchi ikiwa salama.
Waziri Mwigulu ameyasema maneno hayo akiwa kwenye kituo cha STAR TV katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI kinachoratibiwa na kituo hiko kila siku asubuhi kuanzia saa 1:30 mpaka saa 3.