Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete amesema
Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa mahakama ya Afrika ya
haki za binadamu yenye makao yake jijini Arusha ili kuhakikisha kuwa
inafikia malengo ya uanzishwaji wake wa kusimamia haki kwa waafrika.
Rais Dakta Kikwete anatoa kauli hiyo jijini Arusha alipokutana na
wafanyakazi wa mahakama hiyo na kuzindua taarifa za msingi za mahakama
zilizotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ambapo anaongeza kuwa serikali
yake kama mwenyeji wa mahakama tayari imetoa eneo la ekari ishirini
katika eneo la lakilaki wilayani Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa makao
yake ya kudumu.
Akizungumzia umuhimu wa taarifa hizo kuwekwa kwatika lugha ya
kiswahili, rais wa mahakama hiyo ya Afrika ya haki za binadamu jaji
Agustino anasema itaongeza uelewa kwa nchi zinazozungumza kiswahili na
kupanua wigo wa kuitumia mahakama hiyo kupata haki.
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyoanza shughuli zake
rasmi Novemba 2006 baada ya itifaki ya uanzishwaji wake kukubaliwa
nchini Burkina Faso mwaka 1998 ilianzishwa na nchi wanachama wa umoja wa
Afrika kwa lengo la kuimarisha haki za binadamu na watu barani Afrika
na kuimarisha jukumu tume ya Afrika ya haki za binadamu na watu maarufu
kama tume ya Banjul.
0 comments:
Chapisha Maoni