Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Mbuze Masibo mwenye umri wa miaka 76 adaiwa kuwapa dawa inayodaiwa kuwa na sumu watu watano wa familia moja na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mawereru Wilaya ya Geita Septemba 8 majira ya saa tatu usiku ambapo mganga huyo alidai kuwa dawa hiyo inatibu magonjwa mia moja na familia hiyo ikaona ni vyema kunywa kwa kuwa baba wa familia alikuwa akisumbuliwa na vichomi.
Inaelezwa kuwa mganga Masibo alifika katika kaya ya Mabula Sami na kuomba maji baada ya kupewa aliomba apewe hifadhi ya kulala kwani muda ulikuwa umeenda na ataondoka siku inayofuata,baada ya kukubaliwa Masibo alienda msituni na kurudi na mti akidai wa dawa.
Baada ya kunywa dawa hiyo Septemba 9 hali zao zilikuwa mbaya na kukimbizwa katika kituo cha afya ambapo hali zao ziliendelea kuwa mbaya na septemba 10 kukimbizwa hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu walikuwa wakiharisha na kutapika kiasi cha kuishiwa nduvu .
Daktari Hospitali ya Wilaya ya Geita Joseph Edward amesema mara baada ya wagonjwa hao kufikishwa hospitalini hapo hali zao zilikuwa mbaya kwakutapika sana na kuaharisha jambo lililopelekea mmoja kuweza kupoteza maisha.
Waliokunywa sumu hiyo ni Mabula Sami 68, Neema Mabula 11, furaha mabula 5, Rume Mabula 6, Magdalena Rume 50 aliyefariki.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mganga huyo amekamatwa.
0 comments:
Chapisha Maoni