test

Jumapili, 13 Septemba 2015

MAGUFULI ATINGA MKOANI SIMIYU



 Mgombea Urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Lamadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi hao wanaondokana na tatizo sugu la upatikanaji maji.
 Mgombea Ubunge jimbo la Busega Dk. Raphael chegeni akihutubia wakazi wa mji wa maji kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizoongozwa na mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani (kushoto) ,wakipena mikono na Mgombea ubunge wa jimbo la Busega kupitia CCM Dk. Raphael Chegeni wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika mji wa Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu
 Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani akiteta jambo na mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano na wakazi wa mji wa Lamadi, Busega.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi Sapiwi wakati akiwa njiani kuelekea Meatu.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa bariadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa CCM Saba saba.
Wananchi wa Bariadi wakishangilia kwenye mkutano wa mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Maetu kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa atatatua tatizo kubwa la maji kwa kuchukua maji kutoka ziwa Victoria.
 Hivi ndivyo meatu ilibyofurika.




 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr. Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Meatu.
 Wasanii wa Original Komedi wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya stendi Meatu.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Meatu kwenye mkutano wa kumnadi ndugu John Pombe Magufuli.
 Meatu
 Mbunge wa jimbo la Kisesa Ndugu Mhaga Mpina akihutubia wakazi wa kisesa kwenye mkutano uliofanyika Mwandora  ambapo aliwataka wananchi hao kumpigia kura mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani ni kiongozi muadilifu na mpenda maendeleo.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Itilima ndugu Njalu Silanga akijinadi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Nanga ambapo mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.
 Wakazi wa Ikindilo wakimsikiliza mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

 Wakazi wa Bariadi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM saba saba.


Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni