Mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa alishangaza wapinzani wake wakati alipofanya ziara za kushtukiza jijini Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na kupanda daladala, lakini wananchi mkoani Singida walimsaidia kutoa jibu.
Lowassa,
Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne aliyejiondoa CCM
mwishoni mwa Julai, alikuwa akizungumza na wananchi wa Manyoni mkoani
Singida kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Tambukareli.
Katika umati wa watu waliofurika kwenye mkutano huo, kulikuwa na mwananchi aliyebeba bango lililoandikwa “mnashangaa Lowassa kupanda daladala, mbona hamshangai twiga kupanda ndege”.
Wakati
akimaliza hotuba yake, Lowassa aligeuka upande wa kushoto na akaliona
bango hilo likiwa limenyanyuliwa juu. Kabla ya kulisoma alicheka, halafu
akalisoma kwa sauti na kuendelea kucheka, kitu kilichowafanya wananchi
waungane naye kucheka na baadaye kushangilia.
Kabla
ya kuzindua kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa mwezi Agosti, Lowassa alifanya ziara kadhaa za
kustukiza alizozielezea kuwa zililenga kufahamu matatizo ya wananchi.
Alipanda
dalkadala kutoka Gongo la Mboto kwenda Chanika wilayani Ilala,
kutembelea sokoni Tandale wilayani Kinondoni na Mbagala wilayani
Temeke.
Safari zake, ambazo zilipigwa marufuku na taasisi za Serikali, zilimsha mjadala, huku wapinzani wake wakimponda kuwa alikuwa wapi kujua matatizo ya wananchi kabla ya kugombea urais.
Safari zake, ambazo zilipigwa marufuku na taasisi za Serikali, zilimsha mjadala, huku wapinzani wake wakimponda kuwa alikuwa wapi kujua matatizo ya wananchi kabla ya kugombea urais.
Twiga
waliopandishwa ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
na kupelekwa Arabuni waliibwa kwenye moja ya mbuga za mikoa ya
kaskazini, na mtuhumiwa katika kesi hiyo alitoweka nchini na kusababisha
mdhamini wake kuhukumiwa kwenda jela.
Katika mkutano wa jana, Lowassa pia alikabidhiwa funguo iliyoandikwa “Lowassa ni kiboko cha makufuli mabovu”, ujumbe unaolenga kumrushia kijembe mgombea wa CCM, Dk John Magufuli.
Kwenye
mkutano huo, Lowassa alirejea wito wake wa kuwataka wananchi
wanaojitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake wahakikishe wanajitokeza
kumpigia kura ili kuiondoa CCM madarakani.
“Msifurike tu kwenye mikutano, bali mnipigie kura,” alisema Lowassa ambaye alikuwa akishangiliwa wakati wote.
“Nimekuja
kuwaombeni kura kila mmoja wenu anipe. Wakatalieni watakaotaka kuchukua
shahada zenu. Nataka kura zaidi ya milioni 10. Mwambieni shangazi,
mama, baba na hata mshikaji akapige kura na kazi ya pili iwe kuzilinda.”
Mwaka 2010 watu waliojitokeza kupiga kura hawakufika milioni 9, lakini Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakadiria watu milioni 24 kujitokeza kujiandikisha kupiga kura mwaka huu.
Hadi sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijatangaza idadi ya watu waliojiandikisha.
Mwaka 2010 watu waliojitokeza kupiga kura hawakufika milioni 9, lakini Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inakadiria watu milioni 24 kujitokeza kujiandikisha kupiga kura mwaka huu.
Hadi sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijatangaza idadi ya watu waliojiandikisha.
Akizungumzia
matatizo ya wananchi, Lowassa alisema kwa miaka 50 Serikali ya CCM
imeshindwa kuwapa huduma bora na hivyo kilichobakia ni kuiondoa.
“Hamna maji, hampati huduma bora ya afya, kilimo bora hamna, sasa mna nini bora,” alisema Lowassa na wananchi kumjibu, “hamna kitu tunakutaka wewe utusaidie”.
Lowassa
alisema Serikali atakayoiunda itakuwa ya aina yake, na ambaye hataweza
kuhimili vishindo vya utendaji kazi, atakaa pembeni.
“Watu
wanafurika kwenye mikutano yangu mikoani, hii inaashiria kuwa watu
wanataka mabadiliko na hayo yanatakiwa kufanyika katika kura. Kama CCM
wameshindwa kufanya mabadiliko kwa miaka 50 wataweza sasa,” alihoji na kuamsha shangwe kutoka kwa maelfu ya wananchi kwenye mkutano huo,
“Muungano huu (Ukawa) utaleta maajabu, wachagueni watu wetu tulete maendeleo.”
Awali,
Lowassa alimuita jukwaani mgombea ubunge wa Jimbo la Manyoni Mjini kwa
tiketi ya Chadema, Emmanuel Mpandagoya kueleza matatizo yanayowakabili
wananchi wa Manyoni.
“Manyoni tuna tatizo kubwa la maji. Wananchi wameahidi kukupa kura, lakini ukiwa Ikulu kumbuka maji ni kero kubwa hapa,” alisema Mpandagoya akizungumzia tatizo hilo linalozungumzwa karibu katika mikutano yote.
“Pia
tuna tatizo la huduma za afya, ukiwa rais, mimi mbunge wako nitakupigia
simu kukukumbusha kuwa hospitali hazina dawa na baadhi ya vijiji havina
zahanati.
“Tuna
tatizo kubwa la walimu wa masomo ya sayansi na wengi wanaidai Serikali
ya CCM na hawajalipwa madai yao. Hapa Manyoni kila kona watu wanatozwa
ushuru wa bidhaa, umeme umekuwa hadithi. Hizo ndizo kero kubwa za watu
wa Manyoni.”
Akieleza jinsi atakavyomaliza matatizo hayo Lowassa alisema atashughulikia tatizo la maji hadi suluhisho lipatikane.
“Nawahakikishia
wakazi wa Manyoni mkinichagua, kero ya maji itakuwa historia katika
wilaya yenu nitalishughulikia tatizo hili mpaka maji yapatikane,
haiwezekani tangu uhuru hamna maji sasa mnafaidi nini na haya ndio
maisha bora kwa kila Mtanzania?” alihoji.
Kwa
mujibu wa takwimu za Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), takriban
asilimia 80 ya watu wanaoishi mijini wanapata maji ya bomba wakati
takriban asilimia 50 ya watu wanaoishi vijijini ndiyo wanaopata maji ya
bomba. Inakadiriwa kuwa idadi kubwa ya Watanzania wanaishi vijijini.
Awali,
mwanasheria mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki aliyemaliza
muda wake, Tundu Lissu alisema Lowassa analipwa asilimia 80 ya mshahara
wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lakini yeye na wenzake wameamua kujiondoa
CCM na kupoteza stahiki zao nyingi kwa ajili ya kuwapigania wananchi.
“Sumaye na Lowassa wanahangaika na sisi ili watusaidie kuvuka kipande kidogo kilichobakia. Tunachotakiwa ni kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani,” alisema Lissu.
“Sumaye na Lowassa wanahangaika na sisi ili watusaidie kuvuka kipande kidogo kilichobakia. Tunachotakiwa ni kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani,” alisema Lissu.
Lowassa
pia alifanya mikutano Singida Mjini, Kondoa mkoani Dodoma na Ikungi
ambako aliwataka wananchi kumchagua Lissu kwa mara ya pili kuwa mbunge
wa jimbo la Singida Mashariki na kueleza jinsi ilani ya uchaguzi ya
Chadema na Ukawa itakavyokuwa na manufaa kwa wananchi kutokana na
kuwajali wakulima na wafugaji pamoja na elimu kuwa bure kuanzia darasa
la kwanza hadi chuo kikuu.
Mbunge huyo wa zamani wa Monduli leo ataendelea na mikutano mkoani Singida na kesho atakwenda Mkoa wa Shinyanga.
0 comments:
Chapisha Maoni