Wakati
kampeni zikianza, muungano wa vyama vya siasa vinne vya upinzani nchini
UKAWA katika mkoa wa Kigoma umeingia katika mgogoro baada ya kushindwa
kuafikiana kuachiana majimbo matatu ya ubunge baada ya kila chama kuweka
mgombea kinyume na makubaliano ya viongozi wakuu wa vyama hivyo.
Akizungumza baada ya uteuzi wa wagombea katibu wa mkoa wa Kigoma wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Shaban Madede amesema pamoja na ngazi ya taifa ya UKAWA kutoa maelekezo kuwa majimbo ya Buhigwe, Kakonko na Kasulu mjini wapitishwe wagombea kutoka chama cha NCCR mageuzi, Chadema na CUF kimeweka wagombea katika majimbo hayo kutokana na shinikizo la wanachama na kwamba hali hiyo itatatuliwa na viongozi wa juu.

Kwa upande wao viongozi na wagombea katika jimbo la Buyungu Kakonko
wamesema wanashangaa kukiukwa kwa makubaliano hayo jambo ambalo
linaweza kuipa nguvu CCM kushinda katika uchaguzi ujao huku mkurugenzi
wa halmashauri ya Kakonko ambaye ni msimamizi wa uchaguzi katika jimbo
la Buyungu Jaina Msuya akieleza kuwa tayari maandalizi yanaendelea kwa
ajili ya kuhakikisha kampeni zinafanyika kwa amani, aidha pingamizi
kadhaa dhidi ya wagombea katika majimbo ya Uvinza, Kigoma mjini na
Kasulu mjini yametupwa.
0 comments:
Chapisha Maoni