test

Alhamisi, 27 Agosti 2015

Maalim Seif Sharrif Hamad achukua fomu ya urais wa Zanzibar kupitia CUF.


Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharrif Hamad amechukua fomu ya urais huku akimtupia lawama rais wa Zanzibar Dr Shein kwa kushindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wananchi huku mgombea mwengine wa urais wa Jahazi asila akitangaza kuwa yeye ni rais mtarajiwa tayari kwa vile amepewa agizo na mwenyezimungu.
Hali hiyo imejitokeza leo wakati wagombea hao walipochukua fomu za urais ambapo Maalim Seif Sharif Hamad alifika afis za tume akiwa ameambatana na mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chedema Mhe Edward Lowassa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho waliofika kushuhdia tukio hilo la kukabidhiwa fomu na mwenyekiti wa ZEC huku katika hali isiyo ya kawaida maalim alikataa kuondoka hadi fomu hizo zichekiwe na mwanasheria wake ilikuzihakikisha ziko sawa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo Maalim Seif Sharrif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais   alisema tume ya uchaguzi bado haina uwezo na wao hawana imani nayo kwa vile wameshindwa kujipanga na inaendeshwa kwa matakwa ya CCM.
 
Akizungumzia ujio wa serikali ya CUF Maalim amesema ataweka kipaumbele maslahi ya wananchi huku akisisitiza seriklai ya CUF na ile ya UKAWA zitahakishka matakwa ya wananchi kuhusu katiba yana heshimiwa na kufanyiwa kazi.
 
Katika hatua nyengine mgombea urais wa Jahazi asilia Bw Kassim Bakari ali ambaye naye amechukua fomu ya urais katika ofisi za tume na kukabidhiwa na mwenyekiti wa ZEC amesema yeye tayri ni rais mtarajiwa kwa vile amepewa uwezo na mwenyezimungu na ameshapangwa kuwa hivyo.
 
Wagombea wengine wawili wa chama cha Sauti ya Umma na Demokrasia Makni wamechukua fomu za urais na kufanya hadi sasa wagombea waliokwisha chukua ni pamoja na AFP, TADEA, ADC, UPDP, huku CCM ikitarajiwa kuchukua jumatatu asubui.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni