uhamasishaji wa uzazi wa mpango kwa jamii katika maeneo ya starehe ikiwemo kwenye mabaa na vilabu vya pombe mkoani Kigoma.
Mkakati huo unalenga kufikia malengo ya kitaifa ya asilimia 60 ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango ili kuongeza uelewa kwa wananchi ambao wakati mwingine hawafikiwi katika kampeni zinazofanyika.
Akifafanua juu ya mpango huo Meneja Mawasiliano wa Shirika la World Lung Foundation Victoria Marijani alisema mkakati huo umekuwa na mafanikio kiasi katika matumizi ya njia za uzazi wa mpango tangu kuanza kwa kampeni zinazoendeshwa na shirika hilo na watu wameanza kujitokeza katika kutumia njia hizo za uzazi wa mpango.
Nae Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Dokta Leonard Subi alisema bado kuna uelewa wa chini kwa wananchi wa mkoa huo katika kujua elimu ya afya ya uzazi na matumizi ya njia za uzazi wa mpango ambapo kwa sasa asilimia 14 ya wananchi wa mkoa huo ndiyo wanaotumia njia hizo.
Dokta Wilfred Mongo kutoka shirika la EngenderHealth, alisema kuwa bado hakuna wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango na kwamba kilichopo sasa ni watu wengi kutoa habari kuhusu jambo hilo kuliko kutoa elimu.
Alifafanua kuwa dini, mila na desturi pia ni kikwazo kwa wananchi katika kutumia njia za uzazi, ambapo wananchi wengi wanaamini kwamba kila mtoto anakuja na riziki yake aliyoandikiwa na Mungu.
0 comments:
Chapisha Maoni