Wakati Lipumba akiwaambia waandishi wa habari jana kwamba kadi yake ya uanachama bado
iko hai hadi mwaka 2020, akimaanisha kuwa ataendelea kuwa
mwanachama wa CUF nje ya uongozi, taarifa zilizotufikia
zinasema kuwa chama hicho kinajiandaa kumfukuza.
Katika
sehemu ya taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa
habari, Uenezi na Umma wa CUF,Ismai Jussa, inasomeka;
"....Katibu
Mkuu ameagiza kuitishwa vikao vya dharura vya kamati ya
utendaji ya taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa Jumapili,
Agosti 9 2015,kujadili hatua hiyo na kufanya uamuzi juu ya
hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki."
Mpekuzi
imedokezwa kuwa miongni mwa uamuzi unaotarajiwa kufikiwa kesho
na vikao hivyo ni kumfukuza ndani ya chama hicho Profesa
Lipumba.
0 comments:
Chapisha Maoni