KIONGOZI
wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kitendo cha Rais
Jakaya kikwete, kuongeza muda wa bunge kwa siku 10 kwa ajili ya miswada
10 inalenga kupitisha miswada isiyojadiliwa kwa kina.
Amesema
uamuzi huo utaiathiri nchi kwa kuwa wakati huu wabunge wengi
wameelekeza akili zao katika majimbo wanayoongoza, hivyo hawatakuwa na
muda mzuri wa kujadili kwa kina miswada hiyo kwa maslahi ya Taifa
Zitto
alitoa kauli hiyo juzi mjini Kigoma wakati alipofanya mikutano miwili
ya hadhara katika kata ya Nguruka Jimbo la Kigoma Kusini na baadaye
Kigoma Mjini katika uwanja wa Centre.
Alisema
kwa sasa wabunge wana wasi wasi na majimbo yao hivyo kutaka wajadili na
kupitisha muswada wa sheria ya mafuta na sheria ya matumizi yafedha za
mafuta haiwezi kupewa umuhimu na wabunge hao
Badala yake Zitto aliitaka serikali isitishe miswada hiyo mpaka Bunge lijalo wakati wabunge watakapokuwa wametulia "ACT
tunasema miswada hii isubiri Bunge jipya kwani ni miswada muhimu kwa
nchi yetu, miswada inayohusu rasilimali za nchi haiwezi kukimbizwa
haraka haraka bungeni."
Alisema
wasi wasi wa wabunge kwa wakati huu utachangia muswada huo kukosa
umakini Alisema gesi na mafuta yamekaa ndani ya ardhi kwa muda mrefu na
kwamba uharaka wa kujadili miswada hiyo haupo.
Alikumbusha
kuwa Azimio la Tabora lililohuisha Azimio la Arusha linasema wazi sekta
ya madini, mafuta na gesi ni muhimu na zinaweza kuzalisha mapato ya
kutosha ya Serikali ili kuboresha sekta zingine kama kilimo na uwekezaji
katika afya.
"Tunaitaka
Serikali kuchochea mabadiliko makubwa katika sekta hizi za uvunaji wa
maliasili ya nchi kwa kuchukua hatua. "Maliasili zote za madini, mafuta
na gesi ni mali ya wananchi kikatiba na uchimbaji wake lazima uwe na
kibali cha wananchi, mikataba yote iwe wazi kwa wananchi," alisema Zitto.
Alisema
Bunge lilitakiwa kumalizika Juni 27 mwaka huu kabla ya Rais Jakaya
Kikwete kuliongezea siku kumi zaidi kwa ajili ya kujadili miswada hiyo.
Akiwa
katika Kata ya Nguruka Zitto alitumia muda huo kuwatahadharisha watu
wanaotaka kugombea nafasi hiyo nje ya Chama cha ACT-Wazalendo kuwa
wajitafakari mara mbili kama wataweza kupata ridhaa hiyo kwa wananchi.
Aliwaambia
wakazi wa Kata ya Nguruka kama kuna watu wanaona wanakidhi kuwa wabunge
wao watumie jukwaa la ACT-wazalendo vinginevyo wasiwape nafasi hizo.
Aliwatahadharisha wananchi juu ya watu wanaowafikia na kuwaeleza kuwa
watapambana na ufisadi pasipo kuwa na misingi ya kusimamia utekelezaji
huo
"Sisi
ACT-Wazalendo tukisema tunapambana na rushwa tunamaanisha kwa kuwa
tumeweka jambo hili mpaka katika katiba yetu na kisha tukaliweka katika
azimio kwa ajili ya utekelezaji," alisema Zitto.
Awali,
wananchi waliohudhuria mkutano huo waliupokea msafara wa kiongozi huyo
kilomita tano kabla ya kufika Kigoma mjini huku wengi wao wakiwa
wanatembea kwa miguu na wengine wakiwa katika vipande mbalimbali.
Vijana
wa mjini Kigoma walimlazimisha Zitto kushuka katika gari la wazi katika
eneo la Gungu na kumtaka atembee kwa miguu kwa ajili ya kutoa fursa kwa
watu kumsalimia.
Jeshi
la Polisi liliimarisha ulinzi katika misafara hiyo kuanzia mapokezi
hadi kufika uwanjani katika eneo la uwanja baadhi ya watoto walipotezana
na wazazi wao kutokana na umati mkubwa wa wananchi walioshiriki
mapokezi ya viongozi wa Chama hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni