CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Geita kimesema
kimebaini kwa kituo hewa cha kujiandikisha wananchi kwenye daftari la
wapiga kura kiitwacho Buharahara “B” katika kata mpya Bomba Mbili.
Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita, Nguru Tanganyika, alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema
Chadema haikitambui kituo hicho ambacho kipo kinyume na makubaliano
yaliyokuwapo kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Magareth
Nakainga na vyama vyote vya siasa.
Tanganyika
alisema wamekibaini kituo hicho hewa kutokana na jitihada za viongozi
wa chama hicho kutembelea vituo mbalimbali vya kujiandikishia.
“Ofisi
ya Chadema wilaya ya Geita kama mdau wa uchaguzi, imebaini kituo hewa
cha Kata ya Bomba mbili kinyume na makubaliano kati ya Msimamizi wa
uchaguzi ambaye ni mkurugenzi wa Mji wa Geita na vyama vya siasa.
“Tulikubaliana
hakutakuwa na uandikishaji wa wapiga kura Kata ya Bomba mbili kwa kuwa
haijakidhi vigezo vya sheria kufanya uchaguzi kwa sababu ya kukosa
wakazi wanaotosheleza kupiga kura.
0 comments:
Chapisha Maoni