MGOMBEA
anayeomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Steven Wasira, amesema hana majina ya
washukiwa wa ufisadi, ingawa uovu huo umo ndani ya vyama vya siasa
ikiwamo CCM.
Wasira
anayeongozwa na kauli mbiu ya Uadilifu na Umoja wa Watanzania; Safari ya
Uhakika, alisema hayo wakati akizungumza na wana-CCM waliomdhamini
katika mikoa ya Rukwa na Katavi jana.
Alisema CCM na
serikali yake ni taasisi zilizo na misingi ya uadilifu, ingawa ndani
yake kuna uwezekano wa kuwapo watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu huo.
Alisema ufisadi
na rushwa na miongoni mwa matatizo makubwa yanayoiathiri jamii na
kwamba taifa linamhitaji kiongozi asiyekuwa na kashfa inayomfanya
atiliwe shaka katika kukabiliana na kadhia hiyo.
“Hapa sina
majina ya mafisadi lakini ninaamini kwamba si ndani ya CCM pekee, bali
hata katika vyama vingine vya siasa, rushwa na ufisadi ni miongoni ma
matatizo makubwa yanayovikabili,” alisema.
Wasira alisema
kutokana na hali hiyo, vita dhidi ya rushwa na ufisadi inapaswa kuwa
katika misingi ya hoja na uthubutu wa kuidhibiti badala ya kumlenga mtu
binafsi.
Alisema
Tanzania ina taasisi imara ambazo zikitumika ipasavyo zitachochea
kuwatambua washukiwa wa ufisadi, vitendo vinavyoashiria uhalifu huo na
kuchukua hatua kwa ukali na haraka.
Wasira alisema
ikiwa CCM itamteua kuwania na hatimaye kuwania Urais, imani yake ni
katika kutoa uhuru na mamlaka zaidi kwa vyombo husika vikiwamo vya
sheria, kutekeleza majukumu bila kuoneana aibu.
Alisema,
“ninapozungumzia ufisadi sizungumzii mtu au watu, tunauzungumza ufisadi
kama hoja, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hata ndani ya CCM kuna
viashiria vya ufisadi, lakini haimaanishi kwamba CCM ni chama cha
kifisadi.”
Aliongeza,
“hata kwa upinzani kuna ufisadi pia, hivyo ufisadi ni tatizo kubwa
katika jamii yetu, kama nitapata fursa ya kuliongoza Taifa letu
nitahakikisha tunaukabili kwa nguvu zote ili kurejesha heshima na hadhi
ya nchi yetu,” alisema.
Alisisitiza
umuhimu wa kupiga hatua katika kilimo na viwanda ikiwa ni moja ya njia
kuu za kukuza uchumi na kuboresha maisha na ustawi wa wananchi.
Kwa mujibu wa
Wasira, kilimo pekee ndicho kinaweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana
kuliko sekta nyingine pamoja na kuliingizia Taifa pato kubwa zikiwamo
fedha za kigeni.
Wasira
alizungumzia ajira kwa vijana na kusema hivi sasa kuna kasi ya vijana
wengi kukimbia kutoka vijijini kutokana na umasikini unaowakabili, na
kwenda kukutana na umasikini mwingine mijini.
Alisema
uboreshaji wa kilimo, uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya kuongeza
thamani za mazao kutatoa hamasa kwa vijana kushiriki kilimo na
kutengeneza ajira.
Leo Wasira
anatarajiwa kuwasili mkoani Kigoma kutafuta wadhamini, ukiwa ni mkoa wa
30 tangu aanze safari ya kutafuta wadhamini Juni 3, mwaka huu ambapo
alianzia mkoani Dodoma.
Vikao vya
uteuzi vinatarajiwa kuanza mjini Dodoma Julai 5, mwaka huu, ambapo
mgombea urais kwa tiketi anatarajiwa kupatikana Julai 11, na Uchaguzi
Mkuu umepangwa kufanyika mwezi Oktoba.
0 comments:
Chapisha Maoni