Mwigizaji Wema Sepetu na staa wa single ya ‘leoleo‘
Jokate ambao wamekuwa mapenzini na Diamond Platnumz kwa nyakati
tofauti baada ya kutolewa tuzo za KILI 2015 nchini Tanzania ambako Ali
Kiba alipata ushindi wa tuzo nyingi kuliko yeyote mwingine usiku huo
walitumia page zao kumpongeza Kiba kwa kuandika maneno yafuatayo.
Jokate ambaye anatajwa kuwepo mapenzini na Ali Kiba sasa hivi aliandika: "Hongera
Sana Cherie @officialalikiba Kwa Kujishindia Tuzo Sita Jana Usiku
Kwenye Kiba Tanzania Music Awards (KTMA) sorry Kilimanjaro Tanzania
Music Awards 2015. Teh teh teh. Ni Kitu Cha Kumshukuru Mungu Ulikaa
Kimya Miaka 3 Ila Ukarudi Na Wimbo Mmoja Ukatuteka Tena’
"Kusema
Ukweli Tukiachilia Mbali Ushabiki ‘Mwana’ Ulituliza Akili Na Ukafanya
Vizuri Sana Nchini. Mashabiki Wanakupenda. Sana. Mpole Hivi, Mcheshi,
Mstaarabu. Na Unajua Mziki. Tunakuombea Sasa Hii Iwe Motisha Ya Wewe
Kufika Mbali Zaidi. Ndio Kwanza Safari Imeanza. Uzuri Unaomba Mungu So
Najua Hata Kutupa. Ila Kaza Mwana We Kazaaa!!! tuko nyuma yako " – Jokate
Wema Sepetu aliandika : "Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha"
Baada ya Jokate kupost picha ya Kiba na
hayo maneno hapo juu…… post iliyofata aliweka picha yake yeye na Wema na
kuandika: "Ni kitu kizuri na chenye nguvu pale Wanawake hodari wanapoungana"
Ali Kiba mwenyewe baada ya ushindi huu aliandika: “Ningependa
Kuchukua Nafasi Hii Kutoa Shukrani Zangu Kwanza, Kwa MUNGU Muumba
Aliyenipa Kipaji Hiki, Pili Familia Yangu Kwa Kuniongoza Na Kunipa Moyo
Wa Kufanya Kazi Zaidi, My Management, Asante Kwa Kuniongoza Vyema.
Mashabiki Zangu Wa Dhati Asanteni Sana Kwa Kuthamini Kipaji Changu Na
Kupenda Kazi Zangu! Nawapenda Na Kuwashukuru From The Bottom Of My
Heart. MUNGU Awabariki Sana …#KingKiba
0 comments:
Chapisha Maoni