MWILI wa Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unataraji kusafirishwa kesho Jumanne Juni 16, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Akizungumza na
waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania
(Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum, amesema mwili
wa marehemu utaswaliwa kesho katika Msikiti wa Msilimu, viongozi mbalimbali wa
dini na serikali watakuwepo.
Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo.
Hata hivyo amesema
kuwa jana (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Salum amesema
marehem anatarajiwa kuzikwa Alhamis mkoani mkoani Shinyanga .
Sehemu
ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu Mufti Alhaj Sheikh Shabaan
Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
Sheikh
Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana
mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani
kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B leo jijini Dar es Salaam
Kulia
ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa
na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa
Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni