KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye,
amesema katika ziara zote walizofanya katika kipindi cha miaka mitano
bado wananchi wanalalamikia utendaji mbovu kwa baadhi ya viongozi wa
serikali.
Kauli
hiyo aliitoa juzi Wilayani Muleba, alipokuwa akizungumza na wana CCM
ambapo alisema watendaji hao wamekuwa wakishindwa kukamilisha miradi ya
maendeleo.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho wananchi wanaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu
idadi kubwa ya miradi iliyotakiwa kutekelezwa kipindi kilichopita bado
haijamilika.
“Muda
mwingi ambao tumepita kwa wananchi ili kukagua miradi ya maendeleo
tumekuta bado haijakamilika zaidi ya kusikia malalamiko ya wananchi ya
utendaji mbovu wa watumishi wa serikali.
“...
sasa nasema hivi kama wamechoka waondoke, kuna vijana wengi wanataka
ajira hatuwezi kuwavumilia watendaji wabovu ambao kila kikucha wamekuwa
wakirudisha nyuma miradi ya maendeleo kwa wananchi,” alisema Nape.
Alisema
kuna watendaji wengine wakiwaona viongozi wanapita kwenye maeneo yao
wanakasirika, huku wakishindwa kutoa ushirikiano wa miradi
inayotekelezwa katika maeneo yao.
“Kazi
hii ya kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi,
tunayoifanya inawakera baadhi ya watumishi wa Serikali kutokana na
kushindwa kuitekeleza kwa kiwango kilichokubalika,"alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo wanapaswa kukubali kukosolewa pale wanapofanya
makosa ili waweze kurekebisha makosa yao na kuendelea na majukumu yao.
0 comments:
Chapisha Maoni