MAJAMBAZI
watatu wameuwawa katika matukio mawili tofauti Jijini Dar es Salaam,
likiwamo la majambazi wawili kufariki dunia baada ya kujibizana kwa
risasi na Polisi.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Simoni Sirro, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika
eneo la Mbagala Charambe wakiwa na silaha mbili ambazo ni Mark IV yenye
namba 308139 ikiwa na magazine yenye risasi sita.
Alisema
majambazi hayo pia walikutwa na Bunduki moja aina ya Shortgun yenye
namba za usajili TZCAR 356460 ikiwa na risasi saba ndani ya
magazine.
Kamanda
Sirro alisema pia zilikamatwa pikipiki tatu katika eneo la tukio zenye
namba T769 CJW,MC.423ASH na MC982ASG pamoja na simu za mkononi nane za
aina mbalimbali ambazo walikuwa wakizitumia kufanyia uhalifu.
Katika
tukio jingine, wananchi wenyehasira kali wamemuua kwa kumpiga mawe mtu
adhaniwaye kuwa ni jambazi katika eneo la Buguruni jijini dare s salaam.
Kamanda
Sirro alisema jambazi huyo alipopekuliwa alikutwa na silaha aina ya
AK47 yenye namba M73B1-130887 ikiwa na magazine yenye risasi 13 ambayo
ilikuwa ikitumiwa na wahalifu.
Alisema
mafanikio hayo yametokana na oparesheni kabambe ya kuwasaka na
kuwakamata majambazi wa kutumia silaha pamoja na uhalifu mwingine ikiwa
na lengo la kuhakikisha wananchi wanaishi na kufanya shughuli zao za
kila siku bila hofu yoyote.
0 comments:
Chapisha Maoni