MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemwachia huru mtuhumiwa wa kesi ya ukatili dhidi ya mtoto, Georgina Makasi.
Hatua ya kuachiwa huru kwa mtuhumiwa huyo, imekuja baada ya mashahidi upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka.
Mahakama
ilimwachia huru mtuhumiwa huyo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Juma Hassani kwa kuongozwa na wakili wa Serikali, Felista Mosha.
Awali
shtaka hilo lilikuja kwa ajili ya hukumu, lakini mahakama ililazimika
kumwachia huru mshtakiwa kutokana na upande wa mashtaka kushindwa
kuthibitisha ushahidi wao mahakamani.
Juni
6, mwaka 2012, mtuhumiwa Georgina anadaiwa alimpiga mtoto Halima Seif
kwa kutumia pasi ya moto, kinyume cha sheria na haki za mtoto.
0 comments:
Chapisha Maoni