Aliyekuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amekiri
kuumizwa na kashfa mbalimbali zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari
ambazo zilipelekea familia yake kutawaliwa na huzuni jambo ambalo
lilisababisha kuvua taji hilo.
Amesema tuhuma hizo zilimuumiza sana hasa baada ya mdogo wake wa
mwisho kutaniwa na wanafunzi wenzake wakidai kuwa amekuwa akiwadanganya
Sitti, ni dada yake kumbe ni mama yake mzazi.
Amesema kuwa ilifika wakati akiwa anaenda kumchukua mdogo wake
shuleni marafiki wa mdogo wake walikuwa wanamtania wakidai mdogo wake ni
mtoto wa ‘bibi bomba’ wakimaanisha yeye jambo ambalo mdogo wake
lilikuwa linamuumiza sana.
Ameongeza kuwa kuna kipindi mdogo wake alikataa kwenda shule kutokana
na utani kuzidi pia magazeti kuandika kuwa Sitti, ana uhusiano na baba
yake mzazi jambo ambalo lilimuathiri sana mtoto huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni