WAKAZI
wawili wa Kijiji cha Bukigi kilichopo Kata ya Malampaka mkoani Simiyu,
wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na viungo vya binadamu.
Waliofikishwa
juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa mbele wa Hakimu Tumaini Marwa,
ni Matheyo Yumbu (50) na Juma Mihangwa (28).
Ilidaiwa
mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Nassibu Swedy kuwa Mei
5, mwaka huu, saa 11 alfajiri katika Kijiji cha Bukigi, washitakiwa hao
walikutwa wakiwa na viungo hivyo.
Alidai
viungo walivyokutwa navyo washitakiwa hao ni fuvu la kichwa, mifupa ya
miguu na mikono ya binadamu wakiwa wamevihifadhi katika mfuko wa
sandarusi katika nyumba waliyoishi.
Hata
hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo na kunyimwa dhamana na
walipelekwa mahabusu hadi hapo kesi itakapotajwa tena Mei 29, mwaka huu
na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
0 comments:
Chapisha Maoni