Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake
wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo
anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo.
Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu
alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema
Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba.
Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na
mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu
kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye
Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha
ufalme wa Diamond kimuziki.
Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto
wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo
kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya.
“Hamna jipya waache waendelee kumpigia kampeni (Kiba) lakini mimi
nafanya muziki wangu, mashabiki wanafahamu. Kwa hao watoto wa kike,
hakuna kipya kwangu si kimuziki hata maisha yao binafsi.
“Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme. Mwache huyo Kiba aendelee
kula makombo kwa Jokate kama ameamua kipita njia nilizopita si mbaya,
inaruhusiwa,” alisema Diamond.
Jitihada za kumpata Jokate ili aweze kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa
makombo na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu yake kuita bila
kupokewa, jitihada zinaendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni