Wema Sepetu hampendi tena Diamond Platnumz na anasema kila anapoukumbua
uhusiano wao, anakumbuka mambo mabaya zaidi kuliko mazuri.
“Hapana simpendi [Diamond], yalishaisha hayo, nilishampendega, niliwahi kumpenda sana, lakini hamna tena, yaani hata sishtuki,” Wema alikiambia kipindi kifupi cha Kabali cha EFM.
“Nikimkumbuka Diamond most of the things ambavyo ninavikumbuka sio
vitu vizuri na ndio maana hata sasa hivi imekuwa hivyo. Vizuri
vilikuwepo lakini mtu anaweza akafanya vizuri akaja kufanya kimoja tu
kibaya na akaharibu vyote tisa,” aliongeza.
Katika hatua nyingine Wema alisema Zari the Bosslady hamtishi katika sekta ya fashion.
“[Zari] hanitishi kwasababu yeye ana taste yake, mimi nina taste
yangu, yeye ni Zari mimi ni Wema,” amesema muigizaji huyo.
“I got my
own, I like to play along with anything and she got her own.”
0 comments:
Chapisha Maoni