Jungukuu leo
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya,
kimewapiga marufuku wanachama wake wasihudhurie mikutano ya hadhara ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wito
huo umetolewa juzi na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema
(BAVICHA), Wilaya ya Momba, Ayubu Sikagonamo, alipokuwa akihutubia
mkutano wa hadhara katika Kata ya Sogea.
Sikagonamo alitoa agizo hilo baada ya wanachama wa chama chake kudaiwa kupigwa na wanachama wa CCM hivi karibuni.
“Ili
kuondokana na vurugu zinazoweza kuepukika, wanachama wetu mnatakiwa
kutohudhuria mikutano inayoitishwa na CCM, hata kama wamewafuata katika
maeneo mnayofanyia kazi zenu.
“Yeyote
atakayekwenda katika mikutano ya CCM na kupigwa na wanachama wa CCM,
hatutashughulika naye kwa sababu atakuwa amejitakia mwenyewe.
“Wananchi
wote kwa muda huu tunaoelekea kwenye uchaguzi mkuu, kila mmoja awe
tayari kukiunga mkono chama chake na siyo kuwashabikia wengine,” alisema Sikagonamo.
Pia
aliwataka wafuasi wa chama hicho wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili waweze kuwa na sifa za
kuwachagua wagombea wa Chadema na wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Naye
Katibu wa BAVICHA, Wilaya ya Momba, Hoseah Kibwana, alilitaka Jeshi la
Polisi kutokitetea chama chochote cha siasa kwa kuwa hilo siyo jukumu
lake.
Aliwataka
wagombea wa CCM wanaotaka kugombea ubunge katika Jimbo la Mbozi
Magharibi linaloongozwa na Chadema, wasiendelee kupoteza muda kwa kuwa
hawatashinda.
0 comments:
Chapisha Maoni