Chama
cha Mapinduzi (CCM),kinatarajia kufanya vikao vyake mjini Dodoma,ambapo
Mei 22 kitafanyika kikao cha kamati kuu ya CCM,na kufuatia kikao cha
Halmashauri kuu ya CCM Taifa kitachofanyika Mei 23 na 24-2015 mjini
Dodoma.
Akizungumza
na waandishi wa Habari ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi,Ndugu Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku za mikutano
hiyo kunatokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Nape
amesema vikao vyote vikubwa vitafanyika mkoani Dodoma,ambapo ajenda
mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM 2015-2020
ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.
Amesema
kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa
vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya
Mkutano wa Kamati kuu ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).
Nape
amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya
Kikwete katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya
chama hicho.
Wakati
huo huo Nape amesema kuwa wanachama sita waliofungiwa bado hatma yake
kutokana na suala hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo
zinaweza kusema kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe
amezikuta hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na
miongozo ya chama.
Amesema
wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira
yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya
chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema mtu
ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi
yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.
Amesema
mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa
fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa
wagombea kutokana na mazingira yaliyopo
0 comments:
Chapisha Maoni