JESHI
la Polisi Mkoa wa Kagera, linamshikilia Gerald Paulo (34) kwa kosa la
kumpiga binti yake, Anisia Gerald (14), sehemu mbalimbali za mwili wake
na kumyonga kwa kutumia kanga.
Akizungumzia
tukio hilo mjini hapa juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry
Mwaibambe, alisema tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu katika Kijiji
cha Rugazi Kyaitoke kisha alichimba kaburi nyuma ya nyumba yake na
kumzika.
Alisema walipata taarifa kutoka kwa jirani ya Paulo kuwa ameua binti yake na walipofuatilia walibaini ni kweli.
Alisema
baada ya polisi kufukua kaburi hilo walikuta mwili wa binti huyo ukiwa
na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kipande cha kanga
shingoni.
“Kwa
taarifa nilizonazo, Gerald si mara ya kwanza kufanya mauaji kama hayo,
maana miaka mitano iliyopita aliwahi kuua mtu na kukimbilia Karagwe kwa
jinsi hiyo hiyo, kwa tukio hili lazima sheria zichukue mkondo wake,”
alisema Mwaibambe.
0 comments:
Chapisha Maoni