test

Jumanne, 2 Novemba 2021

Nafasi Mpya za Kazi 1097 Mamlaka ya Mapato-TRA... Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 4 November 2021


 


 VACANCY ANNOUNCEMENT

 On behalf of Tanzania Revenue Authority (TRA), Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) invites dynamic and suitable qualified Tanzanians to fill 1097 vacant posts mentioned below.

_________________


1. TAX MANAGEMENT OFFICER II -   NAFASI  294

2. TAX MANAGEMENT ASSISTANT II -NAFASI  326
 
3.CUSTOMS OFFICER II -  NAFASI 167

4.CUSTOMS ASSISTANT II NAFASI 114

5.PUBLIC RELATION OFFICER II – NAFASI  3

6. ICT TECHNICIAN II – NAFASI 30


7. ICT OFFICER II (COMPUTER SYSTEMS ANALYSIS AND DEVELOPMENT) - NAFASI 31.

8. ICT OFFICER II (NETWORK ADMINISTRATOR) –NAFASI  2 

________
 
 ๐Ÿ‘‰Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

9. ICT OFFICER II (DATABASE ADMINISTRATION) - NAFAS 6 .

10. ICT OFFICER II (ICT SYSTEMS RISKS AND SECURITY) – NAFASI 6.

11. ICT OFFICER II (COMPUTER/BUSINESS APPLICATION SUPPORT) –NAFASI 6.

12. ICT OFFICER II (COMPUTER SYSTEM ADMINISTRATION) NAFASI 19.

13. ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) COMPUTER SYSTEMS ANALYSIS AND DEVELOPMENT– 1 POST

14. ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) DATABASE ADMINISTRATION – NAFASI 1.

15.  ICT OFFICER II (BUSINESS ANALYST) SYSTEMS RISKS AND SECURITY-  NAFASI 1 .

16. RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II - NAFASI 18.

17. DRIVER II  NAFASI 59 .

18.  LEGAL COUNSEL - NAFASI 3

19 RATING IINAFASI 1 .

20.ACCOUNTS ASSISTANT II-  NAFASI 4 .

21. PERSONAL SECRETARY IINAFASI 5.

___________________

 Mwisho wa kutuma maombi ni - 4th November, 2021 

 ๐Ÿ‘‰Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>

๐Ÿ‘‰Kupata nafasi mbalimbali za kazi Serikalini na mashirika binafsi <<BOFYA HAPA>>
Read More

Jumamosi, 22 Juni 2019

VEDIO MPYA: Simama na Mungu By Shalom band (Official video)


Read More

Jumanne, 19 Machi 2019

JIFUNZE ZAO LA MAPARACHICHI


Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

1. Faida za Parachichi upande wa Lishe

-Tunda lina vitamini zifuatazo

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

Madini- (Mineral Elements)
Ni tunda lenye

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili


2. Agronomy ya ParachichiHali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasiliKila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi



-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu





-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

UPandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,
-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda
1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni
Jani lililoshambuliwa na Alga


Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia
-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi

-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

 
Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips


DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.


Hitimisho
Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
Read More

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA



 

 

 

 

 

Utangulizi


Mpunga ni zao la pili la chakula kwa umuhimu linalolimwa sehemu nyingi nchini Tanzania. Umuhimu wa zao hili umeongezeka kuanzia muongo uliopita kutokana na jamii za mijini na vijijini kupendelea zaidi kula wali na kupunguza ulaji wa vyakula vingine na kulifanya zao hili kuwa la chakula na biashara.
Mvua ni chanzo kikuu cha maji kwenye kilimo cha mpunga. Viwango vya mahitaji ya maji katika kukua kwa mpunga hutofautiana miongoni mwa aina za mpunga. Ni kwa jinsi hii mpunga hupandwa katika mazingira mbalimbali kutegemea na mahitaji yake ya maji. Zipo aina tatu kuu za mazingira yanayolimwa mpunga kulingana na upatikanaji wa maji na hali ya mwinuko wa nchi. Mazingira haya ni kilimo cha mpunga wa mabondeni kinachotegemea mvua (72%), kilimo cha mpunga wa kwenye miinuko (20%) na kilimo cha mpunga cha umwagiliaji (8%).
Kiasi cha mpunga kinachozalishwa nchini kimekuwa kikiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 41,000 mwaka 1970 hadi tani 811,500 mwaka 1998. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa eneo linalolimwa mpunga na kwa kiasi kutokana na kuongezeka kwa miradi midogo ya umwagiliaji pamoja na matumizi ya tekinolojia bora za kilimo.
Maeneo yanayolima mpunga kwa wingi Tanzania: ni Morogoro maeneo ya bonde la kilombero/Ifakara, Dakawa, Malolo; Mbeya: Kyela, Mbarali; Shinyanga: Kahama; Mwanza, Bonde la Ruvu mkoani Pwani. Na maeneo mengine mengi

shamba-la-mpunga
Shamba la mpunga

pH ya udongo (Soil pH)

pH ni kipimo kinachoonyesha kiwango cha tindikali au nyongo katika udongo. Udongo waweza kuwa tindikali (ph ndogo kuliko 7), nyongo (ph kubwa kuliko 7), au katikati (neutral) - ph ya 7. Tindikali au nyongo ya udongo hupimwa kwa kutumia pH mita. Mazao mengi hustawi zaidi katika udongo wenye hali ya tindikali ya wastani (kipimo cha pH 5.5 hadi 7.0). Mpunga hustawi kwenye udongo wa mfinyanzi wenye tindikali ya wastani na virutubisho vya kutosha.
Kuandaa Shamba, Kupanda na Kupalilia

Kuandaa shamba, kusafisha, kulima/kutifua

Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia:
  • Jembe la mkono - wengi wanatumia
  • Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe
  • Power tillers
  • Matrekta
Baaada ya kulima, shamba linawekwa maji ili liloane vizuri na kisha udongo unachanganywa vizuri na maji ili kutengeneza tope. Hii ni kuchavanga (puddling). Hii inarahisisha:
  • Kupandikiza miche
  • Kuhifadhi maji

Mbegu Bora za Mpunga

Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni:
Mbegu za asili za mpunga: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo. Kuna aina nyingi za mipunga ya asili inayolimwa sehemu mbalimbali hapa nchini kama Supa, Kahogo, Kula na Bwana, Shingo ya mwali, n.k. Wakulima wanazipenda mbegu hizi kutokana na kuwa na sifa kama vile ladha nzuri, uvumilivu wa matatizo mbalimbali ya kimazingira na kwa sababu ya uwezo wa mbegu hizi kustahimili katika hali mbaya ya hewa na hazihitaji uangalizi wa hali ya juu.
Sifa hizi ni matokeo ya mbegu hizi kumudu mazingira na uchaguzi wa mbegu uliofanywa na wakulima kwa miaka mingi. Hata hivyo, nyingi ya mbegu hizi zina uwezo mdogo wa kuzaa, zinachelewa kukomaa, ni ndefu na rahisi kuanguka.
Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutokana na mbegu za asili. Mfano wa mbegu zilizoboreshwa ni kama vile Katrin, IR54, na IR64. Zinazaa sana hasa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, hazikidhi ladha ya walaji na ukobolekaji wake si mzuri na baadhi hazistahimili kwenye mazingira mengi ya kawaida. Hii imezifanya mbegu hizi kukubalika na wakulima kwa kiwango kidogo sana.
Mbegu bora nyingine zilizozalishwa kutoka utafiti na kuonekana kupendwa kwa ajili ya mavuno mengi na ladha nzuri kama TXD88 na TXD85. Hivi karibuni imetolewa mbegu nyingine iitwayo TXD306 (SARO5), mbegu hii hupendwa na wakulima, wafanyabiashara na walaji kutokana na sifa yake ya mavuno mengi, punje ndefu kiasi na nzito, ladha nzuri na yenye kunukia pindi ipikwapo na kuliwa.

Mbolea za kupandia mpunga

Kabla ya kuweka mbolea hakakisha kuwa majaruba yanatengenezwa ili kuhakikisha maji hayaingii na kutoka kiholela. Mbolea ya kupandia huwekwa kwa kusia katika jaruba kabla ya kuchavanga. Kuchavanga husaidia kuchanganya udongo na mbolea na pia kutengeneza eneo zuri la kupandikiza miche. Baadaye miche hupandikizwa.
Viwango vya mbolea za kupandia mpunga
Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 phosphate (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi mifuko mitatu kwa hekta ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari), au mifuko miwili kwa hekta ya Minjingu Phosphate (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari) au mifuko minne na nusu kwa hekta ya Minjingu Mazao (= mifuko miwili kwa ekari).

Jinsi ya kupanda mpunga Kitaalam

Kuna njia mbili kuu zinazotumika kupanda mpunga shambani. Njia hizo ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja shambani na ile ya kupandikiza miche.
  • Kupanda mbegu moja kwa moja
Njia hii hutumika kwa kupanda mbegu moja kwa moja kwenye shamba lililotayarishwa vizuri. Njia ya kawaida waitumiayo wakulima ni ile ya kumwaga na kufukia mbegu (broadcasting). Njia zingine ni zile za kupanda mbegu kwenye mashimo yaliyo kwenye mstari na kwa kuzingatia nafasi maalum au mbegu hupandwa kwenye mashimo bila kufuata mstari na bila kuzingatia nafasi iliyopendekezwa (dibbling). Vile vile mbegu hupandwa kwa kunyunyizwa kwenye vifereji vyenye vina vifupi na kufukiwa pasipo kuwa na nafasi kati maalum kati ya punje na punje (seed drilling)
  • Kupandikiza miche
Njia hii hutumika kwa kupanda mbegu kwanza kwenye kitalu kabla ya kuzihamishia shambani. Mara nyingi mbegu zetu hutumia wiki tatu hadi nne baada ya kuota kwenye kitalu na kufikia umri wa kupandikizwa shambani. Katika shamba la mpunga miche hupandikizwa shambani kwenye mstari na kwa nafasi maalum au kupandikizwa holela bila kuzingatia nafasi maalum za kupanda.
Inashauriwa kupandikiza miche katika kina cha sentimeta 2 hadi 3. Ukipanda kina kirefu machipukizi huchelewa kujitokeza. Baada ya kupandikiza miche, machipukizi hujitokeza baada ya siku 5 hadi 10.
Kupandikiza-miche-ya-mpunga
Kupandikiza miche ya mpunga

Nafasi ya kupanda mpunga

Nafasi ya kupanda mpunga mbegu bora ni sm 15 kwa sm 15 au sm 20 kwa sm 20. Kwenye mpangilio wa mistari miwili miwili (double rows), nafasi kati ya mistari miwili ni sm 10, nafasi kati ya mmea na mmea katika kila mstari ni sm 20, na nafasi kati ya mistari miwili na mistari miwili mingine (double rows) ni sm 40. Mbegu za asili zipandwe kwa nafasi ya sm 20 kwa sm 20 au sm 25 kwa sm 25 au sm 30 kwa sm 30.
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo.

Muda wa kupanda

Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia desemba hadi januari kwa mpunga wa muda mrefu. Kwa mpunga wa muda wa kati na muda mfupi, tarehe ya kupanda ni februari hadi machi.

Kupalilia Mpunga

Ni muhimu shamba lipaliliwe ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno.
Katika kilimo cha mpunga, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Ni vizuri katika kilimo cha mpunga, shamba lipaliliwe mara mbili, kutegemeana na hali ya magugu katika shamba. Unaweza kupalilia kwa kung’olea kwa mkono, kwa mashine au kwa kutumua viua magugu (herbicides) kama vile 2, 4-D (Two Four D).
Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mpunga ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.

Mbolea za kukuzia mpunga

Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni.
Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ya UREA au Minne na Nusu Ya CAN au Mitatu ya SA. Mbolea inayotumika mara kwa mara ni Urea. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium. Kwenye mpunga, mbolea ya kukuzia inawekwa wiki mbili baada ya kupandikiza miche na irudie tena baada ya wiki nne.
Kuweka mbolea: Mbolea ya kukuzia hutiwa kwa kusia wiki mbili baada ya kupandikiza, na kurudia mwezi mmoja baadaye. Ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili ya kiasi kinachopendekezwa.

Mpunga-uliopandwa-kwenye-mistari
Shamba la mpunga uliopandwa kwa mistari

Kudhibiti Magonjwa na Wadudu Wanaoshambulia Mpunga

Magonjwa Yanayoshambulia Mpunga

Magonjwa ya mpunga yamegawanyika katika makundi matatu kulingana na vimelea visababishi ambavyo ni fungasi, virusi na bakteria.
i) Rice blast (Ukungu)
Unaosababishwa na Pyricularia oryzae.
Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies).
ii) Brown leaf spot
Unaosababishwa na Helminthosporium spp.
Dawa/Kudhibiti: Panda mbegu kwa udongo unaofaa, weka mbolea ya kuzuia au tibu mbegu na dawa.
iii) Sheath rot
Unaosababishwa na Acrocylindrium oryzae.
Dawa/Kudhibiti: Kwa sasa hakuna njia ya kuzuia
iv) Rice Yellow Mottle Virus (RYMV) - Kimnyanga
Hivi karibuni ugonjwa wa kimyanga umetajwa kama ugonjwa hatari sana kwa mpunga hapa Tanzania.
Dawa/Kudhibiti: Panda mbegu zilizoboreshwa, zinazostahimili magonjwa au ng’oa mimea iliyoathirika.
Magonjwa yasababishwayo na bakteria nayo wametajwa kuwa na madhara makubwa kwa uzalishaji wa mpunga hapa nchini. Bakteria hawa wanajumuisha Acidovorax avenae subsp. Avenae asababishae ugonjwa wa bacterial stripe, Pantoea aglomerans, asababishae ugonjwa wa palea browning na Xanthomonas oryzae p.v. oryzae.

Wadudu wanaoshambulia mpunga

Kuna aina nyingi sana za wadudu wanaoathiri mpunga katika hatua mbalimbali za ukuaji wa mpunga. Wanapokithiri na wasipodhibitiwa hupunguza kiasi cha mavuno shambani.
i) White flies (Funza weupe)
Dawa/Kudhibiti: Nyunyiza dawa ya Thiodan, Endosulfan (Thionex), Fipronil (k.m. Regent 3G), Fenthion (k.m. Lebaycid)
ii) Rice stalk borer waharibifu
Kudhibiti: Nyunyiza dawa ya Thiodan, Endosulfan (Thionex), Fipronil (k.m. Re­gent 3G), Fenthion (k.m. Lebaycid) Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea na njia zinginezo.

Kuvuna, Kukausha, Kusafisha na Kuhifadhi

Kuvuna: Mpunga uko tayari kuvuna wakati asilimia themanini (80%) ya rangi ya mpunga kwenye masuke imebadilika na kuwa dhahabu. Mpunga unavunwa kwa kukata bua pamoja na suke lake.

Uvunaji-wa-mpunga
Uvunaji wa mpunga
Kukausha: Rundika pahali pakavu k.m. kwenye tuta la jaruba halafu pigapiga (thresh) ili kutenganisha masuke na mpunga. Kama mpunga hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi juani kwa siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mpunga ukauke vizuri ili usioze ukiwekwa ghalani.

Kusafisha: Mpunga uliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mapepe huondolewa. 

Kuhifadhi: Mpunga safi huwekwa kwenye gunia na magunia kupangwa vizuri ghalani juu ya mbao yasiguse sakafu.
Read More

Jumapili, 17 Februari 2019

DAWA 6 ZINAZO TIBU TATIZO LA MWILI KUFA GANZI


Dawa-mbadala-6-zinazotibu-ganzi-mikononi-na-miguuni-520x245

DAWA MBADALA 6 ZINAZOTIBU GANZI MIKONONI NA MIGUUNI

Ganzi mikononi na miguuni inamaanisha kukosekana kwa fahamu katika sehemu hizo. Hisia ndiyo inakosekana sababu kunakuwa hakuna damu na neva zinakosa mawasiliano ya moja kwa moja na ubongo.

Ni jambo la kawaida linalowapata watu wengi sana miaka ya hivi karibuni.

Kinachosababisha ganzi mwilini ni pamoja na:

1. Shinikizo la muda mrefu kwenye miguu na mikono
2. Kuwa karibu na vitu vyenye baridi sana kwa kipindi kirefu
3. Mabadiliko ya muda mfupi kwenye neva
4. Ajali kwenye neva
5. Kunywa pombe kupita kiasi
6. Uvutaji wa sigara na bangi
7. Uchovu sugu
8. Kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara
9. Ukosefu wa vitamini B12 na Magnesiamu
10. Ugonjwa wa kisukari nk

Kwa kawaida ganzi inayotokea kwa dakika kadhaa na kupotea huwa haina shida yoyote lakini onana na daktari mapema ikiwa inakutokea mara kwa mara na pia ikiwa inakutokea na kudumu kwa muda mrefu. Inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa fulani ambao unahitaji matibabu ya haraka.

Kuumwa ganzi kwenye miguu na mikono yako linaweza kuwa ni jambo linaloudhi sana hata hivyo hapa mimi leo nimekuandalia dawa za asili unazoweza kuzitumia kuondokana na tatizo hili.

Endelea kusoma …

Dawa mbadala zinazotibu tatizo la ganzi mwilini:

1. Massaji

Kufanya mazoezi ya massaji wakati unapopatwa na ganzi ni namna nzuri ya kutibu ganzi. Massaji inaongeza msukumo na mzunguko wa damu jambo ambalo mwisho ni tiba kwa tatizo la ganzi. Zaidi masaji inasaidia kusisimua neva na misuli na hivyo kuimarisha na kuongeza mzunguko wa damu kwa ujumla.

*Kwa matokeo ya uhakika weka mafuta ya nazi au ya zeituni au ya mharadali (mustard oil) kwenye viganja vya mikono yako .

*Pakaa sehemu unapopata ganzi

*Massaji maeneo hayo na mikono yako kwa dakika 5 mpaka 7 hivi

*Fanya mara 3 hata 5 kwa siku.

2. Mazoezi ya viungo

Mazoezi husaidia kuimarisha mzunguko wa damu na kuongeza oksijeni sehemu zote za mwili na hivyo kuzuia mwili kupata ganzi.

Mazoezi ndiyo namna pekee ya bure ya kujikinga na kujitibu na magonjwa mengi ikiwemo tatizo la mwili kupatwa na ganzi.

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO GANZI AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5

Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

Mazoezi ya kukimbia, kuendesha baiskeli, kuogelea ni mazuri pia.

3. Bizari

Bizari au manjano ambayo hujulikana kwa kiingereza kama ‘Turmeric’ ina kitu mhimu ndani yake kijulikanacho kama ‘curcumin’ ambacho husaidia kuongeza msukumo wa damu sehemu yote ya mwili wako.

Pamoja na hiyo pia bizari husaidia kuondoa maumivu na hali ya kutokujisikia vizuri katika mwili wako.

Ongeza kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa bizari ndani ya kikombe cha maziwa ya uvuguvugu ongeza kiasi kidogo cha asali na unywe kutwa mara 1.

Unaweza pia kutengeneza uji mzito (paste) wa bizari na maji na utumie kufanya massaji sehemu unapopata ganzi.

4. Mdalasini

Mdalasini una kemikali na viinilishe mbalimbali ikiwemo manganizi na potasiamu na vitamini nyingi za kundi B.

Faida zake za kiafya zinajumuisha pia kuongeza msukumo wa damu kwenye miguu na mikono yako na hivyo kusadia kutibu tatizo la ganzi. Wataalamu wa tiba asili wanashauri gramu 2 mpaka 4 za unga wa mdalasini zitumike kila siku kwa ajili ya kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai ya mdalasini ya unga katika glasi ya maji ya moto na unywe yote mara moja kwa siku.

Au changanya kijiko kimoja kidogo cha chai cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kingine cha asali na ulambe mchanganyiko huu kila siku asubuhi kwa wiki kadhaa.

Angalizo kuhusu mdalasini feki:

Kabla sijakuacha, ni mhimu sana nikueleweshe juu ya mdalasini hasa ambao hutumika kama dawa. Siyo kila mdalasini unaouona unaweza kukupa maajabu haya, mwingine ni sumu kabisa mwilini. Na watu wengi hawajuwi hili jambo.

(a) Ceylon cinnamon

Mdalasini ambao hutumika kama dawa hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Ceylon cinnamon’ na kwa kawaida wenyewe huuzwa gharama sana. Huwa na radha tamu na harufu ya kuvutia zaidi, unatoka katika nchi ya Sri Lanka katika mmea ujulikanao kama Cinnamon Zeylanicum. Hujulikana pia kama mdalasini wa India.

Huwa na rangi ya kahawia (light brown), mwembamba na mlaini.

(b) Cassia cinnamon

Wakati ule ambao ni feki na ni sumu pia hujulikana kama ‘Cassia cinnamon’ ni mdalasini huu ambao katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku kutumika wala kuingizwa nchini mwao. Hujulikana pia kama mdalasini wa China na wengine huuitwa Saigon.

Mdalasini huu unatoka katika nchi za China, Vietnam na Indonesia. Wenyewe huwa una joto zaidi na huwa na radha kali nay a kuwasha ukiutumia. Madhara yake ni pamoja na kudhuru Ini na figo ukitumika kwa kipindi kirefu.

Cassia cinnamon huuzwa bei rahisi sana na mwingi unaopatikana huko masokoni ni huu. Huwa na rangi inayokaribia na uweusi.

Kwa kawaida ni vigumu kutofautisha aina hizi mbili za mdalasini ukishakuwa tayari katika mfumo wa unga tofauti na ukiwa bado katika fimbo au magome. Mhimu tu ni ununuwe kutoka kwa mtu unayemuamini zaidi.

5. Kula zaidi vyakula vyenye vitamini B

Ili kuzuia ganzi mwilini hasa kwenye mikono na miguu ni mhimu kwamba unakula vyakula zaidi vyenye vitamini B kwa wingi hasa vitamini B6 na B12.

Vitamini hizi ni mhimu kwa ajili ya afya nzuri katika kuzipa neva uwezo wa kufanya kazi vizuri na upungufu wake unaweza kusababisha ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye mikono, vidole, na miguu.

Vyakula hivyo ni pamoja na mayai (mayai ya kuku wa kienyeji), parachichi, nyama, maharage, samaki, maziwa, mtindi, mbegu mbegu nk

Unaweza pia kutumia vitamini B-complex mara 2 kwa siku kila siku. Kwa dozi sahihi zaidi muulize daktari wako wa karibu.

6. Ongeza matumizi ya magnesiamu

Usawa mdogo wa magnesiamu katika mwili ni moja ya sababu ya kutokea kwa ganzi katika sehemu mbalimbali za mwili. Magnesiamu ni madini mhimu katika kuwezesha ufanyaji kazi ulio mzuri wa neva za mwili na mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Kula vyakula vyenye magnesiamu zaidi kama vile mboga majani zenye rangi ya kijani, mbegu mbegu, siagi ya karanga, soya, parachichi, ndizi, chokoleti nyeusi, na mtindi wenye mafuta kidogo.

Unaweza pia kutumia viinilishe vya magnesiamu gramu 350 kila siku ila ongea kwanza na daktari wako wa karibu.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia

1. Kuwa bize na mazoezi kila siku
2. Usikae muda mrefu kwenye kiti
3. Epuka chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine vyote vyenye kaffeina
4. Kula zaidi matunda na mboga za majani
5. Kunywa maji mengi kila siku kidogo kidogo kutwa nzima
6. Epuka sigara na bidhaa nyingine za tumbaku
7. Vaa viatu ambavyo ni saizi yako pia epuka viatu vyenye visigino virefu zaidi
8. Hakikisha una uzito sahihi na siyo uliozidi

Mawasiliano zaidi: WhatsApp +255769142586

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao
Read More

DAWA MBADALA YA KURUDISHA UKE ULIO TANUKA AU KUREGEA


Tokeo la picha la embe
 Jinsi gani ya kukaza uke au ni namna gani kufanya uke uwe mdogo tena ni mada au somo lisilopendwa kuzungumzwa na watu wengi.

Ikiwa wewe ni mmoja wa waathirika na tatizo hili basi tumia muda wa kutosha kusoma makala hii sasa hivi, irudie mara nyingi mpaka umeielewa.

Kwenye makala hii nakwenda kukuonyesha baadhi ya mbinu za jinsi gani ya kurudishia tena uke mkubwa au uliolegea na kuwa mdogo tena ukiwa nyumbani bila kuhitaji kutumia matibabu mengine ya bei kubwa.

KINACHOSABABISHA UKE KULEGEA

Uke kulegea au kuwa mkubwa zaidi unaweza kutokea kutokana na sababu nyingi. Kumbuka pia kushiriki tendo la ndoa mara chache siyo suluhisho la kuwa na uke mdogo. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kuwa na uke mkubwa na kushiriki tendo la ndoa mara nyingi.

Pia hakuna uhusiano wa umri na ukubwa wa uke. Wapo wamama watu wazima wana uke mdogo pia kuna wasichana wadogo kabisa wana uke mkubwa kupitiliza.

Kama ilivyo kwa uume kwamba wanaume wana uume wenye ukubwa tofauti tofauti kadharika wanawake nao kila mwanamke ana uke wa ukubwa tofauti tofauti tofauti.

Kwa kawaida hakuna mwanaume anayependa kushiriki tendo la ndoa na mwanamke mwenye uke mkubwa. Kuna tetesi zisizo rasmi kuwa hata wanaume wanaopenda kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile na wake zao huanza tabia hiyo mara baada ya kuona uke umelegea kiasi cha kutokuwa na radha tena.

Uke kulegea ni matokeo ya asili ya kuchakaa na kupanuka kwa kuta zake.

Mfano mara baada tu ya kujifungua misuli ya uke inalegea na kama hutachukua hatua mapema uke unaweza kupoteza hali ya kujibana tena na kurudi kwenye saizi yake ya awali.

Sababu kuu za uke kulegea na kuwa mkubwa ni pamoja na:

* Kuzaa mara kwa mara
* Uzito na unene uliozidi
* Kujifungua kwa upasuaji
* Kuinua vitu vizito mara kwa mara
* Mazoezi mazito ya mara kwa mara
* Misukosuko ya siku za nyuma katika nyonga
* Ukomo wa hedhi
* Maumivu sugu nyuma ya mgongo
* Kupiga chafya au kikohozi mara kwa mara
* Kufunga choo au kupata choo kigumu mara kwa mara

Mlolongo huu ni wa asili, hata hivyo kuna hatua unaweza kuzichukua na hivyo kurudishia kifaa chako katika hali ya kawaida kama msichana tena.

Baadhi ya wanawake hupendelea kufanya upasuaji maalumu ili kurudishia maumbile yao kuwa madogo jambo ambalo linaweza kuwa na athari kubwa kiafya hapo baadaye.

Zipo njia za asili unazoweza kuzifuata kukusaidia kukaza tena kifaa chako ukiwa nyumbani na kwa namna za asili bila kukuacha madhara yoyote hapo baadaye.

Ili kufanya misuli ya uke ibane unaweza kutumia njia zifuatazo. Ukiweza jaribu njia 2 mpaka 3 tofauti kwa siku kwa matokeo yenye uhakika zaidi.

Mbinu mbalimbali zinazotumika kurejesha uke mkubwa au uliolegea

1. Kula chakula sahihi

Moja kati ya njia nzuri zaidi za kupunguza ukubwa wa uke ni kula mlo sahihi ambao utasaidia kujenga afya ya misuli na kuta za uke kwa ujumla.

Kwa mjibu wa watafiti ni kuwa unatakiwa ule zaidi vyakula vyenye kuhamasisha uzalishwaji wa homoni ya estrogen vyakula kama uwatu, komamanga, ufuta, maharage ya soya na bidhaa zake, karoti, tufaa (apple), viazi vikuu (yams) nk.

Vile vile hakikisha unakula vyakula vya asili zaidi na siyo vya dukani au kwenye makopo au kwenye migahawa.

Matunda fresh yanaweza kukusaidia kuwa na harufu nzuri ukeni na kuwa na uke wenye afya. Vile vile kunywa maji mengi kila siku iendayo kwa Mungu na hivyo utakuwa na shepu nzuri ya mwili wako.

2. Jeli ya mshubiri freshi

Kutumia jeli ya mshubiri au aloe vera ni moja ya njia rahisi ya asili ya kukaza uke wako. Kutumia njia hii kwangua jeli (utomvu mweupe) wa ndani wa jani la mmea wa mshubiri ukiwa freshi na upake sehemu yote ya ndani ya uke wako mara 2 mpaka 3 kwa siku kwa wiki 3 hadi 4 na hutakawia kuona matokeo mazuri.

Matumizi ya jeli ya aloe vera kusaidia kupunguza uwezekano wa uke kulegea.

Aloe Vera ni dawa asili iliyothibitika kukaza uke kwa asili bila madhara yoyote mabaya. Ina vitamini nyingi zikiwemo vitamini A, C, folic acid, choline na madini kama zinki, magnesiamu, kalsiamu na sodiamu vyote hivi ni mhimu katika kuhamasisha kukazika kwa uke kwa ujumla.

Mmea huu wa asili hauna ugumu wowote katika matumizi yake. Tumia tu jeli kutoka katika jani freshi la mu-aloe vera na utumie vidole vyako kusambaza ndani ya uke.

Kama jeli hii ikichanganywa na mate kabla ya kupaka ukeni inaweza kutumika kama dawa bora ya kulainisha pia uke mkavu na kufanya tendo la ndoa lenye kuvutia sana.

Nina uhakika kuwa hii siyo mara yako ya kwanza kusikia kuhusu kazi hii ya mmea huu. Mshubiri unatumika katika bidhaa nyingi za vipodozi za asili.

3. Zabibubata (Gooseberry)

Zabibubata ni moja ya dawa asili nzuri zaidi katika kukaza kuta za kifaa chako. Chemsha kwenye moto zabibubata 10 mpaka 12 ndani ya maji upate kama supu hivi nzito. Kisha mimina kwenye chupa safi na utunze sehemu safi na salama.

Pakaa hiyo dawa kila siku ndani ya uke wako dakika 10 kabla ya kwenda kuoga. Hii itaongeza uwezo wa kujibana tena kwa misuli ya kifaa chako.

Kwa hakika zabibubata ndiyo moja ya dawa asili za kubana uke wako tena ambazo unatakiwa uzijaribu huku ukiongeza matunda haya kwenye chakula chako kila mara.

4. Mtindi

Njia nyingine nzuri ya kushughulika na tatizo hili ambayo nataka kukufunulia kwenye makala hii kwako wewe msomaji wangu ni matumizi ya mara kwa mara ya mtindi. Hii ni kwa sababu mtindi unao bakteria wazuri wanaohitajika ili kuuacha uke katika afya nzuri muda wote. Vile vile ukitumia mtindi kila siku ni namna nzuri ya kutibu maambukizi mbalimbali katika uke.

Kikombe kimoja kwa siku (robo lita) inatosha. Unaweza pia kuweka kijiko kidogo kimoja cha chai cha mtindi ndani ya uke wako wakati unaenda kulala na uusambaze vizuri sehemu yote ya ndani ya uke wako.

Mtindi unaweza kutumia wa nyumbani au hata ule wa dukani ni sawa.

5. Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu kinaweza kuwa msaada katika kutibu baadhi ya maambukizi yaliyosababishwa na fangasi. Kutumia kitunguu swaumu mara kadhaa kwa wiki inaweza kuwa njia nyingine nzuri katika kusaidia uke wako kubaki salama na wenye afya.

Vile vile kitunguu swaumu husaidia kuondoa harufu mbaya katika kifaa chako.

* Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
* Kigawanyishe katika punje punje
* Chukua punje 3 au 4
* Menya punje moja baada ya nyingine
* Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
* Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

6. Mbegu za uwatu

Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha tumbukiza vijiko vikubwa viwili vya mbegu za uwatu ndani yake na ufunike kisha acha kwa usiku mzima mpaka asubuhi.

Asubuhi kunywa hayo maji na ule hizo mbegu pia. Fanya zoezi hili mara 3 TU kwa wiki na uenndelee na zoezi hili mpaka kifaa chako kimerudi na kuwa kidogo. Hii inasaidia pia kupunguza uzito.

Mhimu – Wanawake wajawazito au wenye saratani ya matiti wasitumie dawa hii.

7. Unga wa mbegu za embe

Unga wa mbegu za embe ni dawa nyingine nzuri unaweza kutumia kukaza misuli ya uke wako uliolegea. Ukishakula embe chukua ile kokwa yake ya ndani na uianike juani, ikikauka chukua na uisage upate unga wake.

Changanya unga huu na asali kidogo kisha pakaa ndani ya kuta na sehemu yote ya ndani ya uke kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa na uke wako utarudi na kuwa wa kawaida.

Mbegu za embe ni chanzo kizuri cha wanga, mafuta, protini, vitamini E, nyuzinyuzi, magnesiamu, vitamini B12, asidi amino nyingi nk.

8. Vitamini E

Kwa mjibu wa utafiti kuhusu faida za vitamini E ni moja ya vitamini mhimu sana ambazo ni mhimu kwa ajili ya afya bora ya mwili. Inapendekezwa kama dawa ya kutibu kisukari na shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito.

Hata hivyo wanawake wengi hawafahamu ukweli kwamba vitamini E ni dawa nzuri kwa uke mkavu na kufanya kuta za uke zenye afya na nguvu kama itatumika vizuri.

Unahitaji upate mafuta ya vitamini E na uwe unaweka ukeni moja kwa moja mara 1 kwa siku mpaka utakapopata uponyaji unaouhitaji. Huwa kama kidonge hivi lakini ni mafuta na kinapasukia chenyewe ndani ya uke na kusambaa bila shida yoyote.

9. Umhimu wa kufika kileleni

Moja kati ya njia nzuri zaidi zinazoweza kupelekea uke kukaza ni kuhakikisha unafikishwa kileleni unaposhiriki tendo la ndoa.

Watafiti wamethibitisha pasipo na shaka kuwa wakati mwanamke anapokuwa anafika kileleni misuli yake ya ukeni hujikaza na kujifinya vya kutosha tendo linalofanya uke kujikaza na kuwa mdogo kwa asili.

Fanya utafiti. Kama una tatizo la kuwa na uke mkubwa kuna uwezekano mkubwa tatizo halihusiani na sababu nilizozitaja hapo juu. Kuna uwezekano mkubwa hufikishwi kileleni kwa kipindi kirefu au kwa miaka mingi tangu uanze kushiriki tendo la ndoa.

Kama mwenza wako hajuwi ni dalili zipi mwanamke huwa nazo anapofika kileleni mwambie anitafute nitamsaidia kumwelewesha.

10. Fanya mazoezi yafuatayo

KEGEL – Wakati unakojoa mkojo wa kawaida uwe unajizuia kwa sekunde 10 au 15 kisha unaendelea hivyo hivyo, yaani unakojoa kidogo unaacha kwa sekunde 10 tena unakojoa hivyo hivyo huku unapumzika mpaka unamalaiza.

Fanya zoezi hili mara 3 mpaka 4 kwa siku ukienda kupata haja ndogo. Zoezi hili kwa mjibu wa watafiti ni kuwa linasaidia kukaza misuli ya uke.

SQUATS – Hili ni zoezi lingine zuri la kubana uke uliolegea. Ni kusimama na kuchuchumaa, kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo mara 15 kwa mizunguko mitano mara 2 kila siku. Zoezi hili linasaidia pia kuwa na maungo mazuri na faida nyingine nzuri za kiafya.

LEGS UP – Lala chali kisha nyanyua mguu mmoja juu kisha shusha chini na unyanyuwe mguu mwingine juu na ushushe chini hivyo hivyo mguu mmoja juu kisha chini, kisha mwingine juu chini ukichoka unapumzika kisha unaendelea hivyo hivyo kila siku kwa dakika 15 mpaka 20 mpaka kifaa chako kitapokuwa sawa.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia:

*Kuwa msafi kila mara
* Vaa nguo za ndani zinazotengenezwa kwa pamba
* Usitumie pafyumu zenye kemikali

Njia hizi nilizozielezea hapo juu zote ni nzuri katika kurejesha katika saizi ndogo uke ulikokwisha kuwa mkubwa au uliolegea. Chakula na mazoezi pia ni mhimu kuzingatia kwa matokeo mazuri na yenye uhakika.

Wakati mwingine unaweza kuchelewa kuona mabadiliko lakini usikate tama mpaka umefanikiwa. Kwahiyo kama wewe ni mmoja wa watu wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili usiichukulie poa hii makala jaribu yaliyopendekezwa humu na uniletee mrejesho.

Ikiwa utahitaji dozi kamili ya dawa hizi basi niachie tu ujumbe WhatsApp +255769142586 muda wowote mimi nitakujibu.

Kuna dawa nyingine tofauti na hizi umewahi kutumia na zikakusaidia? Kama ndiyo nitajie hapo chini kwenye comment kwa faida ya wengine.

Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya uwapendao

Read More

Mbinu 10 za kuongeza mbegu za kiume (sperm count)


Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote.

Visababishi vya mbegu kuwa chache:

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:

• Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume.

Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

• Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta.

Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

Vingine vya kuviacha ni pamoja na bangi na madawa mengine yote ya kulevya.

• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako.

Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

• Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.

Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku.

Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

• Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto.

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vingine ni pamoja na kuendesha baiskeli masaa mengi, kukosa muda wa mazoezi ya viungo na kutoshiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.

MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME (sperm count)

1. Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu tatizo lako.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Hii inaweza kusaidia kutibu tatizo lako la kuwa na mbegu chache kwa haraka sana.

Endelea kusoma zaidi hii makala hapa chini.

2. Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Navyo ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti nk.

Hivi vitu vyenye kaffeina ni sababu ya kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume.

3. Tumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe. Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu viwili mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Kitunguu swaumu kina kitu kingine kiitwacho ‘Allicin’ ambacho huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Ongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usizidishe zaidi ya punje 3 kwa siku.

4. Kula ndizi

Ndizi hazifanani tu na uume kama unavyoweza kuwaza bali pia ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Ndizi pia zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Kula mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi ccha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Pia mbegu za maboga zina kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.

Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.

Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia

Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.

Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.
6. Kula zaidi mboga za majani

Mama alikuwa sahihi kumbe ingawa nilikuwa nachukia nikikuta mboga majani badala ya nyama nikirudi kutoka shule.

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote.
Tokeo la picha la parachichi
Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 5 hivi na huwa nazichanganya na chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

Unaweza pia kuzisaga na mashine maalumu au kuzitwanga katika kinu na utapata unga wake na utumie vijiko vikubwa viwili kutwa mara 1 kwenye kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au katika uji.
7. Kunywa maji mengi kila siku

Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama wala ugomvi wowote kukuelewesha. Mwenyewe unajua kuwa maji ni uhai na kuwa asilimia 75 ya mwili wako ni maji, sasa kama huna tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku sijuwi unategemea miujiza kutoka wapi.

Huhitaji kusikia kiu au mpaka upate hamu ya kunywa maji bali hili ni jambo la lazima kwamba huwezi kukaa bila kunywa maji halafu ubaki na afya bora.

Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu.

Kama utatekeleza mengine yote niliyoelekeza hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umeshachemka tayari.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

8. Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Katika utafiti mmoja wanaume walioongeza utumiaji wa folic asidi na zink waliongeza uwingi wa mbegu zao kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wiki 2 tu.

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti.

Hivyo isipite siku bila kula parachichi 1 kutafuna karoti moja kama una tatizo la mbegu chache.

Vingine ni pamoja na mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

9. Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.

Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.

Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.

10. Spinach

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.

Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi upande wa mwanamke (birth defects) kama ujauzito kutoka mara tu mimba inapotungwa.
Read More

Kwa wewe mwanaume mwenye tatizo la kufika kileleni haraka kabla mpenzi wako hajaridhika




Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.


Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.
Kimsingi mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.

Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

Kupiga punyeto au kujichua;
Mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabia ile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa;
Kukaa muda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. Kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa;
Mtu akiwa na historia ya kupata hali hii kabla, huwa hajiamini na kuwa na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu;
Baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

Kurithi;
Baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kuwa na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.

Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.

Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.

Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.

Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.

Punguza wasiwasi:
Hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu, hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.

Fanya taratibu:
Picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.

Badilisha style:
Ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.
Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa

Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
Hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.

Fanya na kuacha:
Hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
Hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

Tumia kilevi:
Unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.

·
Matibabu ya kutumia dawa.
Hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...

1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.[dawa hizi hazipatikani ndani ya nchi hivyo tunaagiza nje, ukihitaji wasiliana nasi kwa namba hapo chini]

2. anesthetic creams: hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.

Read More

VYAKULA 7 VINAVYO ONGEZA NGUVU ZA KIUME


606fa6b4770b61100b57487b4945b0468647f69b
Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.


Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.



Sababu za kukosa nguvu za kiume

 Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?

Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:

Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya TestosteroneKupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini


Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano na ndoa.


1. Blueberry



525719769


Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.


Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.



2. Mtini (Figs)



fig-wasp-3

Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.


3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)



oysters

Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.


Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.



4. Karanga

peanuts-in-shell

 

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.



5. Vitunguu saumu



Garlic-cloves---do-you-kn-008

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.



6. Ndizi



Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).



7. Chocolate



Right-Way-to-Melting-Chocolate

Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.



Vyakula ni bora kuliko madawa makali

Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.


Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.


Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.


Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.
Read More