Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
uteuzi wa Athumani Selemani Mbuttuka kuwa wa Msajili wa Hazina.
Taarifa
hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson
Msigwa imesema kuwa uteuzi wa. Mbuttuka utaanza Juni 6, 2018.
Aidha,
kabla ya uteuzi huo, Mbuttuka alikuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Taifa (DAG) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali
(NAOT).
Mbuttuka anachukua nafasi ya Dkt. Oswald Mashindano ambaye tayari amekwisha staaafu.
0 comments:
Chapisha Maoni