Mahakama
ya Mji wa Kampala nchini Uganda, imempata na hatia mwanamke mmoja
aliyejulikana kwa jina la Amina Mirembe (23) baada ya kukiri kosa la
kujiteka makusudi kwa lengo la kupima upendo kwa mume wake.
Gazeti
la Daily Monitor, limeripoti kuwa mwanamke huyo amehukumiwa jana Juni
5, 2018 kwa kutoa taarifa za uongo kwa Polisi kuhusu kutekwa kwake na
Hakimu wa Mahakama hiyo Patrick Tulisana alimhukumu kwenda jela mwaka
mmoja na kutoa kiasi cha shilingi za Uganda 300,000.
Mwendesha
mashtaka wa serikali, Bi Lydia Batiibwe aliitaka Mahakama kutoa adhabu
kali kwa mtuhumiwa Amina ili iwe fundisho kwa watu wanaotoa taarifa za
uongo huku nchi hiyo ikikumbwa na matukio mengi ya kujiteka makusudi
Mei
26, 2018 mshtakiwa aliandika maelezo ya uongo kwa Askari Polisi ASP
Moses Acaye, katika eneo la Ntinda na kudai alikuwa ametekwa na watekaji
hao walikuwa wakitaka shilingi za Uganda 500,000
Nchini
Uganda kumekuwa na matukio ya watu kujiteka na kudai fedha kutoka kwa
watu wa karibu, mathalani Juni 4, 2018 makahama eneo la Kayunga,
ilimpata na hatia Bi Rebecca Birabwa (32) kwa makosa ya kujiteka na
alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela .
0 comments:
Chapisha Maoni