Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kukaa pamoja na chama cha
wapangaji wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kusikiliza
changamoto zao pamoja na kutoa fursa kwa wapangaji wa muda mrefu kununua
nyumba hizo.
Mhe.
Majaliwa ametoa tamko hilo leo Bungeni, Jijini Dodoma alipokuwa akijibu
swali la Mbunge wa Ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu juu ya lini Serikali
itakutana na wanachama na wamiliki wa nyumba za NHC ili kutoa fursa kwa
wapangaji wa muda mrefu kuzinunua nyumba hizo badala ya kuwaondoa.
“Shirika
la nyumba inayo sera inayotoa muongozo namna nyumba hizo zinavyotakiwa
kutumika ikiwemo na maamuzi kwa wale wanaokaa kwa muda mrefu kwenye
nyumba hizo inapofikia thamani ya nyumba kushuka iweze kurasimishwa
rasmi ili kutoa fursa kwa wapangaji hao kuweza kuzinunua kwa kulipa
kiwango kidogo kidogo,” alisema Waziri Mkuu.
Aliendele
kusema, asilimia kubwa ya wapangaji wa muda mrefu wa nyumba hizo ni
wastaafu ambao hawana nyumba. Hivyo ameitaka NHC kuangalia jambo hilo na
kuwapa fursa wapangaji hao kulipa kidogo kidogo kadiri ya uwezo wao.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotumia
lugha ya kuudhi au kutumia nguvu pindi wanapokusanya kodi kwa
wafanyabiashara. Badala yake wawaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu
wa kulipa kodi na kuwaeleza ni kwa kiasi gani kodi hiyo imefikia.
Amesema
hayo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduma Mhe. Frank
Mwakajoka kuhusu kauli ya Serikali juu ya usumbufu unaoletwa na TRA kwa
wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi.
“Serikali
imeunda chombo cha kusikiliza kero za wananchi ndani ya TRA lakini kama
hawatasikilizwa wanauwezo wa kupeleka kero zao Wizara ya Fedha au kwa
kiongozi yoyote mkubwa katika eneo lake kama vile Mkuu wa Mkoa au
Wilaya,” alisema Waziri Mkuu.
Aidha
ameitaka Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa na mazungumzo na
wafanyabiara. Pia tathmini ya kodi isiwe kiwango kikubwa kuliko mtaji wa
mfanyabiashara.
Hata
hivyo amesema hatua zitachukuliwa kwa yeyote ambaye hatatumia utaratibu
mzuri wa kukusanya kodi na amewataka wafanyabiashara kufanya biashara
kwa amani.
0 comments:
Chapisha Maoni