Licha
ya kumaliza msimu kwenye nafasi ya tatu ambayo ni mbaya zaidi kuwahi
kuwatokea katika miaka ya hivi karibuni, Yanga imekumbana na kasheshe
jingine ambalo limefanya mambo yao kuwa mabaya zaidi.
Simba
na Azam zimeamua kuanzia vurugu zake za usajili katika kikosi cha
Yanga ambapo zote mbili zimeikomalia kwelikweli huku mastaa wakubwa wa
Jangwani wakionekana kupagawa na mafungu waliyowekewa mezani.
Usajili
rasmi unaanza Juni 15 lakini Simba na Azam zimeanza kuvuna Jangwani.
Kwanza Yanga walikuwa wanamtaka Adam Salamba kutoka Lipuli, lakini juzi
jioni aliwashangaza wengi baada ya kutua Simba kwa kile kilichodaiwa
kuwa Yanga walishindwa kufikia dau linalotakiwa.
Simba
wamempa Salamba Sh40milioni taslimu na jana Jumanne walimkabidhi gari
ya kutembelea aina ya Crown mpya yenye thamani ya zaidi ya Sh15milioni.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, limeeleza kuwa linafahamu
kuwa wachezaji muhimu wa Yanga wanaondoka na kujiunga Azam na Simba na
kilichobaki ni ishu ya muda tu kwani wameshashawishika.
Wachezaji
wanaotarajiwa kuondoka ni Papy Kabamba Tshishimbi, Kelvin Yondani,
Hassan Kessy na Obrey Chirwa huku Donald Ngoma yeye akiwa ameshasaini
Azam, kila mmoja ataondoka kwa dau lake na sababu kubwa ni ukata na
maisha magumu ndani ya Yanga ambapo hawapati sapoti yoyote kwa wadau
kama awali.
Lakini nje ya Yanga Simba wanaweza kuwanasa pia, Pascal Wawa na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United.
PAPY TSHISHIMBI:
Huyu
bado ana mkataba wa mwaka mmoja kwa sasa, lakini Simba wamepania
wanamtaka na wana nia kweli, muda wowote unaweza kusikia chochote.
“Huwezi
kuamini hata y e y e mwenyewe a n a t o a ushirikiano m k u b w a kwa
Simba na hata l e o ( j a n a ) tutawasiliana nae tena,”alisisitiza
kiongozi mmoja makini wa Simba.
“Huyu
Simba wanaweza kuwapa Yanga hata milioni 100,hela ipo sasahivi, Yanga
wanatafuta hela ya kusajili,”kiliongeza chanzo chetu cha uhakika.
Hata
hivyo, imefahamika kuwa mchezaji huyo naye anataka kuondoka kwenye timu
hiyo kutokana na hali ya kiuchumi kuwa mbaya hivyo anaweza
kuwashawishi viongozi wake wakavunja mkataba na kujiunga na timu hiyo.
Tshishimbi
alisaini mkataba wa miaka miwili na sasa amebakiza mwaka mmoja tu na
kuna baadhi ya vitu kwenye mkataba wake ambavyo inaelezwa Yanga
hawajavitimiza ambavyo vinaweza kumruhusu akauvunja mkataba huo.
KELVIN YONDANI
Awali ilikuwa inaelezwa kuwa Simba wanamtaka beki huyo lakini kibao kimebadilika na sasa anaweza kwenda kujiunga na Azam.
A
n a y e t a r a j i w a kuwa kocha mpya w a A z a m kuanzia msimu
ujao, Hans van Pluijm amepende k e z a jina la beki huyo m w e n y e
uwezo wa juu kuwa asajiliwe na timu hiyo.
H
a t a hivyo, hakuna kizuizi chochote kinachomzuia kwenda kwenye timu
hiyo kwa kuwa hadi sasa yeye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na
Yanga kumalizika.
HASSAN KESSY
Hakuna
aliyekuwa a n a f i k i r i k u h u s u H a s s a n K e s s y k w e n
d a A z am, l a k i n i m a m bo yanaelezwa kuwa y a m e b a d i l i k
a baada ya beki aliyekuwa anatakiwa na timu hiyo Juma Abdul kugoma
kuondoka Yanga, ndiyo wakaweka nguvu kwa Kessy ambaye naye h a n a mk a
t a ba na timu hiyo ya Jangwani.
Kessy
anawadai Yanga na wala hajasaini mkataba hadi sasa, Azam
wameshazungumza naye na kuna uwezekano mkubwa akasaini wiki hii kwa
kuwa kila kitu kinaonekana kuwa tayari kukamilika alisema mtu wa karibu
na Kessy.
PASCAL WAWA
Kwa
mashabiki wa soka la Tanzania wanamfahamu beki huyo kisiki raia wa
Ivory Coast, lakini habari ya kushtua ni k w a m b a a n a k u j a
nchini na k u s a i n i S i m b a mwaka mmoja.
Simba
wanamtaka Wawa kwa kuwa wanafahamu kuwa ana uzoefu wa kimataifa na
atawasaidia sana msimu ujao ambao wanaingia kwenye michuano ya Klabu
Bingwa Afrika.
Wawa
amemalizana na timu yake ya sasa El Merreikh ya Sudan na ameshafanya
mazungumzo ya awali na kiongozi mmoja wa Simba na inaelezwa katika
mazungumzo yao mchezaji huyo amesema anahitaji mshahara tu kwanza apige
kazi bila fedha yoyote ya usajili.
Inaelezwa kuwa akiwa Sudan alikuwa anaendelea kuwa mchezaji tegemeo kama wakati akiwa na Azam.
TAFADZWA KUTINYU
Habari
nyingine njema kwa mashabiki wa Azam, ni kwamba klabu yao imepindua
meza na tayari imekamilisha usajili wa kiungo wa Singida United,
Mzimbambwe Tafadzwa Kutinyu.
Awali
uongozi wa Singida ulionekana kuweka ngumu mchezaji huyo kujiunga na
Azam lakini mwenyewe alishinikiza kuwa anataka kuondoka na kwenda Azam.
Kocha
Pluijm alishindwa kumshawishi kuendelea na timu ya Singida kwa kuwa
timu hiyo inashiriki michuano ya kimataifa na hivyo akasema anakwenda
Azam lakini kwa mzuka wa viongozi wa Azam walionao lolote linaweza
kutokea.
Siyo
kimataifa tu hata fedha kwa kuwa ingekuwa ni hivyo angesubiri Singida
wacheze na Mtibwa fainali ya Kombe la FA kwani wangeweza kupata nafasi
hiyo lakini yeye alisisitiza kuwa anataka kwenda Azam na inasemekana
amesajiliwa Azam kwa gharama ya dola 20 , kilisema chanzo kutoka
Singida.
OBREY CHIRWA
S
i m b a w a m e shasema k u p i t i a msemaji wao Haji Manara kuwa
watakwenda nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa na jina kubwa
kwenye mic h u a n o hiyo zaidi ya Salamba na taarifa zinasema kuwa
wapo karibu sana kumalizana na Chirwa ambaye mambo yake yanasimamiwa na
Jonas Tiboroha.
Habari
zinasema kwamba Chirwa anataka kutua Msimbazi na ana nafasi kubwa ya
kumrithi Laudit Mavugo ambae bado yupo Sinza, Dar es Salaam anakula
bata lakini ameshapigwa chini.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kuna vita kubwa sana kati ya Simba na Azam kuhusu mchezaji huyo.
Ofisa
Habari wa Simba alisisitiza jana Jumanne kwamba; “Tutalipiza kila aina
ya kisasi walichotufanyia wakati ule. Kwenye usajili tunafuata
maelekezo ya Kocha lakini kuna sehemu fulani siasa za usajili
zinaruhusiwa, unachomeka kidogo kumuumiza mtani wako.”
“Nakwambia
tutashtua, kuna jina moja kubwa tunakwenda nalo Nairobi. Nakwambia
tutashtua. Hao ambao mmeshawasikia mpaka sasa ni chamtoto,”alisisitiza
Manara ambaye amekuwa ni mtu mwenye furaha kwa madai kwamba Yanga
iliwazingua sana enzi za Mwenyekiti Yusuf Manji.
0 comments:
Chapisha Maoni