Rais
Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba endapo Marekani itajiondoa kwenye
mkataba wa nyuklia kati ya nchi yake na mataifa yenye nguvu duniani,
basi Marekani itajutia maisha yake yote.
"Ikiwa
Marekani itaondoka kwenye makubaliano ya nyuklia, mutaona hivi karibuni
watakavyojutia kuliko ilivyowahi kuwatokezea kwenye historia," alisema
mwanamageuzi Rouhani kwenye hotuba yake ya jana (Jumapili 6 Mei) akiwa
kaskazini mwa Iran.
"Trump
anapaswa kujua kuwa watu wetu wameunganika, utawala wa Kizayuni
(Israel) unapaswa kujuwa kuwa watu wetu wako kitu kimoja," alisema
Rouhani.
"Leo,
mirengo yote ya kisiasa nchini Iran, ama iwe kulia au kushoto,
wahafidhina, wanamageuzi na watu wa mrengo wa kati, wote wameungana,"
aliongeza.
Rais
Donald Trump wa Marekani ametishia kujiondoa kwenye makubaliano hayo
wakati utakapofika muda wa kusainiwa upya tarehe 12 Mei, akiwataka
washirika wa Ulaya "kuyarekebisha makosa makubwa yaliyomo" ama sivyo
arejeshe upya vikwazo dhidi ya Iran.
Mkataba
huo wa nyuklia ulisainiwa mwaka 2015 kati ya Iran na Uingereza, China,
Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Marekani, wakati huo ikiongozwa na Barack
Obama.
Chini
ya makubaliano hayo, vikwazo vilipunguzwa kwa masharti ya Iran
kutokuunda bomu la nyuklia, lakini Iran inasema haioni mafanikio ya
ahadi hizo licha ya kutimiza masharti ya mkataba.
Mara
kadhaa, Rouhani amekuwa akirejelea msimamo wa nchi yake kupinga
kuzuiliwa nchi yake kuunda makombora yasiyo ya kinyuklia, na hilo
amelizungumzia pia kwenye hotuba yake ya Jumapili.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kushoto) anaamini kuwa Marekani haina sababu ya kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran.
Naye
Trump amekuwa akiukosoa mkataba huo, akitaja baadhi ya vifungu ambavyo
anasema vinaondoa vikwazo vya nyuklia kuanzia mwaka 2025.
Macron aonya dhidi ya vita
Katika
jitihada za kuyaokoa makubaliano hayo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
amependekeza hivi karibuni kwamba mkataba huo utanuliwe kuyashirikisha
masuala kama hayo yanayolalamikiwa na Trump, na pia kuondoa kikomo ya
muda wa Iran kuruhusiwa kuunda makombora mengine na pia kuangalia dhima
ya Iran kwenye eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati.
Hatua
ya Iran kumuunga mkono Rais Bashara al-Assad, kupitia kundi la
Hizbullah la Lebanon, na pia kuwaunga mkono waasi wa Kishia nchini Yemen
kumeongeza mzozo kati yake na mataifa ya Magharibi.
Licha ya hayo, jana Rais Macron ameonya kwamba kunaweza kuzuka vita endapo marekani itajiondoa kwenye makubaliano hayo.
"Tunaweza
kuibuwa mambo mengine mapya. Kunaweza kukawa na vita," Macron
ameliambia gazeti la kila wiki la Ujerumani, Der Spiegel, ingawa
ameongeza: "Sidhani kama Donald Trump anataka vita."
0 comments:
Chapisha Maoni