Kijana
Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika
kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya
mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa
kuuiba kung’ang’ania mabegani.
Wakati
akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa
kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro,
Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo
Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi
ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine,
ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani.
Ameendelea
kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke
kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini
aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda
mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije
akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amesema walilazimika kumtafuta mhusika wa mzigo huo ili kuweza kumsaidia kijana Frank Joseph ambaye aliiba kiroba hicho, baada ya wao kushindwa kumtua.
Kamanda Shanna ameendelea kusimulia kuwa wakati wakijaribu kumtua kijana huyo kiroba cha mahindi alichoiba alikuwa akilalamika kupata maumivu makali, na ndipo wakamsaka mmiliki wa mzigo ili kumsaidia.
0 comments:
Chapisha Maoni