Mbunge
wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka waziri wa
Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue.
Amesema
hayo bungeni leo Aprili 12, 2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya
bajeti ya Ofisi ya Rais, yenye wizara za Tamisemi; na Utumishi na
Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Habari
zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo, sisi
watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo
mlielewe,” amesema.
Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya.
Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika.
“Familia
imechukua hatua mbalimbali, imelalamika na sisi wajumbe wenzake
tumehoji kwenye vikao, hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,” alisema
Zitto.


0 comments:
Chapisha Maoni