Msanii
wa Bongo movie Wema sepetu amefunguka tena kuhusiana na wasanii wenzake
kumtolea povu baada ya kujishindia tuzo mbili kama msanii bora wa kike
katika tuzo za SZIFF.
Wasanii
kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo
cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna wasanii
wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.
Baada
ya povu hilo Wema amewajia juu wasanii hao na kuwataka waache wivu
kwani yeye amestahili tuzo hiyo kwa movie yake ya heaven sent kwani
imeleta changamoto kwa wasanii wenzake.
Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Wema alifunguka haya:
"Kwanza
kikazi kidogo tu cha heaven sent kimeleta maneno haya...kwahiyo
wamenitia hasira na pia wamenifanya nione kuwa mimi ni tishio kwao,
alafu huyo mtu ambaye anaongea nimesha fanya naye kazi alafu tumeshawahi
kuwa karibu
"Mimi
sina tatizo na yeye nashangaa kwa Nini imekuwa hivi halafu nimeshafanya
naye movie na nimemnyoosha kwenye kazi ambayo tumefanya lakini sijawahi
kusema kitu chochote kibaya juu yake”.
Wema
ameongeza kuwa kinachosababisha mpaka mambo yanakuwa hivi ni wasanii wa
Bongo movie kuoneana wivu ambao unasababisha kunakuwa hakuna umoja kati
yao hali inayosababisha tasnia hiyo kurudi nyuma.
0 comments:
Chapisha Maoni