Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk Philipo Mpango amesema utaratibu wa kujibu hoja
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ulikuwApo toka
siku nyingi, lakini haukuwa wa kwenda mbele ya vyombo vya habari.
Dk
Mpango ametoa kauli hiyo leo Aprili 13, wakati akijibu maswali ya
waandishi wa habari katika utaratibu wa mawaziri kujibu hoja za CAG, leo
ilikuwa zamu ya mawaziri wa habari na viwanda.
Amesema
zamani kulikuwa na utaratibu wa Serikali kujibu kwa kuweka taarifa hizo
bungeni, lakini wameona haifai kwa kuwa mwenzao CAG anaweka bungeni
kisha kuita vyombo vya habari.
"Hakuna
kukaa kimya, tunatumia sheria ya ukaguzi wa umma namba 418 (38) kifungu
kidogo cha 3, Serikali inatakiwa kujibu na sasa tumeanza kujibu kwa
kutumia njia anazotumia." amesema Dk Mpango.


0 comments:
Chapisha Maoni