Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Mhagama amefunguka na kutoa ushauri kuhusu suala la
maandamano na kusema kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima
afuate sheria hata kama maandamano yanatambulika kikatiba.
Jenista
Mhagama amesema hayo bungeni na kudai kama kila mtu ataamua kuandamana
kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu hilo
litakuwa jambo ambalo si sawa hivyo amevitaka vyama vya siasa kufuata
sheria za nchi na si kuvunja sheria za nchi.
"Suala
la maandamano katika nchi yetu ya Tanzania linaratibiwa na sheria za
usalama ndani ya nchi chini ya vyombo vya usalama hasa polisi na Katiba
haiwezi kuchukuliwa kwamba ni kigezo cha kuviruhusu vyama kufanya
maandamano bila kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.
"Ninaomba sana Watanzania wote na niviombe vyama vyote vya siasa katika nchi yetu ya Tanzania wahakikishe wanazingatia sheria.
"Katiba
yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na
kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria
katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania"
Jenista Mhagama aliendelea kutoa maelezo kuhusu masuala ya maandamano
"Labda
niulize swali moja tukiamka hapa siku moja asubuhi na kila mtu ameamua
kuandamana wakulima, wafanyakazi yaani kila mtu aamue tu kuandamana kwa
sababu tu Katiba imesema nadhani itakuwa siyo sawa na nichukue nafasi
hii kuviomba vyama vya siasa kuheshimu Katiba na sheria katika
kutekeleza wajibu wao na siyo kuvunja sheria za nchi yetu Tanzania"
0 comments:
Chapisha Maoni