Wachunguzi wa kimataifa leo Aprili 18 wameingia katika mji wa Syria uliokumbwa na kile kinachodaiwa kuwa ni shambulizi la sumu.
Hata
hivyo, wachunguzi hao wanaingia nchini humo ikiwa ni siku kadhaa za
kucheleweshwa na onyo kutoka kwa mataifa ya magharibi kuwa ushahidi
muhimu huenda umeshaondolewa.
Shirika
la habari la Syria - Sana limesema wataalamu hao kutoka Shirika la
Kimataifa la Kudhibiti Silaha za Sumu -OPCW wameingia mjini Douma.
Shambulizi hilo linalodaiwa kuwa la gesi mnamo Aprili 7 mjini Douma, karibu na Damascus, liliripotiwa kuua zaidi ya watu 40.
Mataifa ya magharibi yalimtuhumu Rais wa Syria Bashar al-Assad kwa tukio hilo.
Watalaamu hao waliwasili Syria siku ya mashambulizi ya nchi za magharibi lakini wakazuiwa kuingia Douma.
0 comments:
Chapisha Maoni