Wabunge
wa wametakiwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti vitendo vya unyanyasaji
wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto wenye ulemavu
katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Ushauri
huo umetolewa mara baada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa na shirika
la ‘Action On Disability and Development’ kwa kushirikiana na
shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania kubaini kuwepo kwa vitendo vya
udhalilishaji wanawake na watoto wenye ulemavu.
Akizungumza
na Wabunge katika semina iliyoandaliwa na Shirika la ADD, Mjini Dodoma,
Mkurugenzi wa Shirika hilo Rose Tesha amesema kuwa baadhi ya ndugu na
jamaa wamekuwa wakishiriki vitendo hivyo hususani kwa watoto wenye
ulemavu wa kusikia na akili.
Aidha,
Wakitoa maoni yao katika Semina hiyo baadhi ya wabunge wametaka sheria
iweze kurekebishwa ili mfuko wa jimbo pia uweze kuwahudumia watu wenye
ulemavu huku wengine wakitaka uboreshaji wa miundombinu kwa watu wenye
ulemavu.
0 comments:
Chapisha Maoni