Mamlaka
ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja changamtoto tano za
uendeshaji kesi zinazotokana na makosa ya mtandao.
Changamoto
hizo zimetajwa kuwa ni uelewa mdogo wa majaji, mahakimu na wanasheria,
ushahidi wa kuwasilisha, kufutika kirahisi, uchunguzi, na wapi pa
kupeleka malalamiko hayo.
Mwanasheria
mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Philikunjombe amewataka majaji na
mahakimu na wanasheria kupata elimu juu ya uendeshaji wa kesi hizo kwani
kumekuwa na makosa makubwa yanayotendeka.
Mbali
na hiyo amesema bado kuna ugumu wa kujua ni namna gani ushahidi
unatakiwa kuwasilishwa mahakamani pindi mtu atakapokwenda kulalamika
kuwa katendewa makosa.
”Umetukanwa
kwenye simu je upeleke simu ya aliyekuwa kwenye simu, je upeleke simu
ya aliyekutukana mahakamani, Tutajuaje kama baada ya kumnyang’anya simu
yake hukubadilisha ujumbe. Kama umechapisha katika karatasi, tutajuaje
kama hukuongeza maneno au kupunguza? Hivyo, bado ni vigumu kupata
ushaidi wa kesi hizi” amesema Philikunjombe.
Lakini
pia changamoto nyingine ni ushahidi wa kesi hizo kuharibika kirahisi
kwa sababu mtuhumiwa anaweza kufuta ujumbe hivyo haitakuwa rahisi
kuthibitisha makosa hata kama ujumbe huo utakuwa nao mlalamikaji.
Kufuatia
changamoto hizo wadau mbalimbali wanaotumia mitandao wameshauri
wasimamizi wa kesi hizo kupewa elimu ya sheria zinazohusu makosa ya
mtandao ili haki iweze kutendeka.
0 comments:
Chapisha Maoni