Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema katika
mikakati yake ya kuwatambua wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI
pamoja na TB wameazimia kutembea maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi
ikiwemo baa, migodini na mahali penngine ili waweze kuwatambua
kiurahisi.
Hayo yameelezwa na serikali ya awamu ya tano kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Aprili 23, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 15 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza kutoka kwa Mbunge Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.
"Serikali baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB".
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo lipo kwenye mikakati ya serikali katika kufufua uwezo wa kufikia watu wote wanaohitaji huduma za TB ili kuwagundua mapema na kuwatibu kikamilifu.
0 comments:
Chapisha Maoni