Wabunge
wa upinzani wakiwamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ni
kama wamesusia Mkutano wa 11 wa Bunge ulioanza vikao vyake mjini Dodoma
jana huku viti vyao vikionekana vitupu.
Aidha,
kutokana na kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
(Chadema), swali laki ilibidi liulizwe na Mbunge wa Liwale, Zuberi
Kuchauka (CUF).
Wabunge
hao wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ambapo jana wabunge waliokuwapo
walikuwa wanne tu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) na wabunge wawili wa
Chadema.
Hata
hivyo, leo wabunge wa Chadema hawakuwapo kabisa ambapo baadaye
walionekana wabunge wawili tu, akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na
Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili ambao walionekana kwa muda mfupi
kwa nyakati tofauti na kupotea.
Kubenea
aliingia bungeni asubuhi na kutoka kabla ya kikao kuanza huku Kamili
akionekana nje ya ukumbi wa bunge bila kuingia ndani.
Wabunge
wa CUF walikuwapo lakini idadi yao ikiwa haifiki 20 wakati wa kipindi
cha maswali na majibu na kubaki tisa pekee baada ya kipindi hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni